"Ukiwa meneja wangu nitashinda hadi Grammy" Lady Jaydee amwambia Steve Nyerere

Lady Jaydee ndiye mwanamke ni miongoni mwa wanawake waanzilishi wa miziki aina ya Bongo Fleva.

Muhtasari

• Nyerere alimtaka Jaydee kurudi kweney gemu la bongo fleva kwa kile alisema kwamba uwepo wake kimuziki unakosekana sana.

Mwenyekiti wa ndoa ya Billnas na Nandy, Steve Nyerere
Screenshot Mwenyekiti wa ndoa ya Billnas na Nandy, Steve Nyerere
Image: Clouds FM

Msanii mkongwe malkia wa muziki wa Afrika Mashariki, Lady Jaydee amemtaka muigizaji Steve Nyerere kuwa meneja wa kazi zake za muziki huku akisema kwamba hilo likifanikishwa basi atazikwaa ngazi hadi kushinda tuzo maridadi zaidi duniani ya Grammy.

Jaydee alikuwa akijibu maoni ya Steve Nyerere kwenye ukurasa wa muigizaji huyo wa Instagram alikopakia picha za pamoja baada ya kukutana na mwanamuziki huyo.

“Jana Nami nilipewa Bahati ya kuonana na Mwanamke bingwa Hapa Tanzania katika Mziki, Yani mfungua njia @jidejaydee lakini nikaongozana na Baunsa wangu @edokumwembe,” alisema Steve Nyerere.

Muigizaji huyo ambaye ana umaarufu mkubwa kutokana na kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa hafla mbalimbali za tafrija alizidi kusema kwamba tangu Jaydee aweke muziki pembeni kidogo kwa kupunguza kasi ya kuachia vibai, bado kuna pengo kubwa sana ameliacha na kumtaka arudi kwenye muziki.

“Hakika Dada bado Watanzania wanakuhitaji,..Kikubwa Natamani Nichukue Jukumu la kusimama nawe, Asante sana Dada, Na Yajayo yanafurahisha Kikao kimeisha salama, hivi karibuni Dada ana jambo lake,” Nyerere alidokeza tukio kubwa linalotarajiwa kutoka kwa mwanamama huyo.

Hapo ndipo Jaydee alimmiminia sifa na kumtaka awe meneja wa kazi zake za muziki kwani hilo ndio hakikisho tosha kwamab atanyakua tuzo mbalimbali kwenye ulingo wa muziki kote duniani.

“Naomba uwe meneja wangu , nahisi tutapata hadi Grammy,” Jaydee aliandika.

Baada ya picha hizo za kupendeza za Jaydee, watu mbalimbali walimpongeza kwa kujitunza vizuri huku wengine wakisema walianza kumsikiliza kitambo sana ila inafurahisha kumuona bado anang’aa mpaka sasa wakati watu wa umri wa nyuma wamezidi kupatwa na mapeto mwilini.

“Dah!, kumbe yupo tu fiti mpaka sasa. Nakumbuka niko darasa sijuwi langapi nilipenda sana sauti yake kwa zile nyimbo: Anita yeye na Matonya na Kisa sio pombe,” shabiki mmoja aliandika.