"Siwezi lala chumba kimoja cha hoteli na mke wangu!" - Bien Aime wa Sauti Sol

Msanii huyo alidokeza kwamba wakienda shoo mkewe anakuwa meneja wake na hivyo hawawezi lala pamoja.

Muhtasari

• Alisema mkewe ni meneja wa kazi zake za kimuziki na hivyo hata wakiitwa shoo basi uchumba unabaki nyumbani.

Bien Aime na mkewe Chikki Kuruka
Bien Aime na mkewe Chikki Kuruka
Image: Maktaba//RadioJambo

Msanii mkongwe kutoka rekodi lebo ya Sol Generation, Bien Aime kwa mara nyingine tena ameibuka na kauli zingine zenye utata kuhusu uhusiano wa ke na mkewe mtangazaji Chikki.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee kwenye kituo kimoja cha redio humu nchini siku chache zilizopita, msanii huyo alisema kwamba katika ndoa yake kuna changamoto nyingi kama ndoa nyingine nyingi tu kwani huwezi zungumzia ndoa na ukwepe suala la changamoto.

Kama msanii Harmonize ambaye meneja wa kazi zake za muziki, Bien Aime pia alifichua kwamba mkewe ndiye meneja wa kazi zake za kibinafsi, kando za zila wanazofanya kikoa kama kundi la Sauti Sol.

Alisema kwamba wakati amealikwa kutumbuiza katika tamasha au hafla au hata tafrija inayomhitaji kulala, huwezi kumtengea chumba cha kulala pamoja na mkewe hata kama ni meneja wake, alisema hawezi kulala kweney chumba kimoja na kitanda kimoja na mkewe kwani anajua hapo shughuli iliyompeleka ni kujitathmini ni jinsi gani atakavyotumbuiza jukwaani.

Msanii huyo alisema kwamba yeye hutaka kutengewa chumba chake maalumu mbali na kila mtu akiwemo mkewe na hata muziki usiwepo kwa sababu anataka kuchukua fursa hiyo kujisikiliza na kujiandaa tayari kwa kutikiza jukwaa.

“Katika ndoa yetu kuna mipaka pia, kwa mfano kama nimeitwa mahali niko na shoo, nakaa kwa chumba cha hoteli mimi peke yangu. Huwa sitaki hata muziki hapo ndani. Nataka tu kukaa peke yangu nijisikilize na kujitathmini kuhusu jinsi nitakavyoifanya hiyo shoo. Kwa hiyo kama unaniita kama ajenti ama promota, huwezi nitengea chumba kimoja mimi na mke wangu, sitaki kulala na yeye kitanda kimoja hiyo siku, nataka kuenda kujisikilizia,” Bien alisema kwa mshangao wa wengi.

Alifafanua kwamba wakienda kwa shoo na mke wake mambo ya uchumba yanabaki nyumbani na kule wanaenda kama msanii na meneja wake na kwa hiyo kuna umuhimu wa kila mmoja kutengewa chumba chake binafsi mbali na mwingine.

Hii si mara ya kwanza msanii huyo anaibua kauli kinzani kwani hivi majuzi tena katika mahojinao mengine alinukuliwa akikiri kwamba yupo tayari kuenda kufanya mpango wa uzazi wa vasektomia kwa ajili ya mkewe, kuliko mkewe kufanya mpango wa uzazi wa sindano au tembe.