(+video) Jacky Vike Awinja amfanyia kuku wake 'babyshower', amvalisha kitenge

Jacky Vike alisema kuku huyo wake anaitwa Perpetua

Muhtasari

• Katika hafla hiyo pia alimleta jogoo aliyekuwa amevalishwa nadhifu hadi tai na kusema ni mumewe Perpetua - kuku wa kike

• Hii inakuaj siku chache tu baada ya dadake Betty Kyallo, Glory Kyallo kumfanyia mbwa wake babyshower

Muigizaji Jacky Vike almaarufu Awinja Nyamwalo amewaacha wanamitandao katika kicheko kirefu baada ya kumfanyia kuku wake tafrija ya kutarajia kutotoa vifaranga, kwa kimombo ‘Baby Shower’

Katika video ndefu ambayo Awinja aliipakia kwenye YouTube yake, anaonekana akiwa na kuku huyo kike ambaye amemvalisha nguo nzuri huku akisema anaitwa Perpetua.

Video hiyo ya ucheshi mkubwa inaonesha watu kadhaa wakiwa wamehudhuria hafla hiyo ambayo Awinja alisema ni siku kubwa ya kuku wake Perpetua akitarajia kuangua vifaranga.

“Karibu kwa babyshower ya Perpetua. Mwanzo ningependa kusema ahsanteni sana kwa kuja, niliwaita na mkaitikia wito, ingawa kuna wengine hawakuja,” alisema Awinja.

Pia alionekana muigizaji mwenzake Osoro kutoka kundi la waigizaji la Mkisii ni Mkisii akiwa na jogoo ambaye pia alikuwa amevalisha nadhifu mpaka tai huku wawili hao wakisema kwamba kuku hao ni mke na mume.

Waigizaji waliokuwa katika klipu hiyo waichukua fursa hiyo na kutoa ushauri kwa wanandoa hao ambao ni kuku huku wakiigiza kwa uhalisia kabisa utadhani ni mawaidha yanayotolewa kwa wanandoa kabla ya kuruhusiwa kuenda fungate.

Ingawa kisa hiki Awinja alikifanya kama klipu cha kuchekesha tu, il ani kimoja ambacho kinawakumbusha Wakenya kuhusu hulka ambayo inaendelea kuchukua mizizi miongoni mwa wakenya wenye ‘nacho’ kuandaa tafrija za haiba ya nyota tano kwa Wanyama wao wa kufugwa nyumbani.

Wiki mbili zilizopita, dadake mwanahabari mashuhuri Betty Kyallo, Glory Kyallo aligonga vichwa vya habari baada ya kuandaa babyshower kwa ajili ya mbwa wake ambaye alikuwa anatarajia kuzaa kwa mara ya kwanza.

Siku chache baadae, mtangazaji mashuhuri nchini Kamene Goro naye pia alidokeza kwamaba atarusha tafrija la aina yake kwa ajili ya mbwa wake wa kufugwa nyumbani.

Hii hulka inaendelea kushika kasi licha ya Wakenya wengi haswa walala hoi kuendelea kuonekana kuikemea kwa kile wanasema kwamba katika uhalisia wa utu, binadamu anafaa kumsitiri mwanadamu mwenzake na Wanyama kuja baadae lakini hawa wanakiuka utaratibu huo na kuandaa tafrija kali kwa ajili ya Wanyama wa kufugwa hali ya kuwa Jirani zao pengine wanalala njaa katika hali ya uhayawinde uliopitiliza.

Yepi maoni yako kuhusu Wanyama wa kufugwa kufanyiwa tafrija za kifahari?