(+video) Justina Syokau: Nataka Ringtone arudi kwa injili tuoane, nilivunjika moyo alipoasi injili

"Bado namuombea Mungu amrudishe kwenye muziki wa injili" - Justina alisema

Muhtasari

• "Jambo moja ninalopenda juu yake ni kwamba alikuwa na maudhui mazuri. Ringtone alikuwa akiimba kwa njia nzuri," Syokau alisema

Mwanamuziki mwenye utata, Justina Syokau amefunguka kwamba mapenzi yake kwa msanii Ringtone bado yapo na pindi aliposikia kwamba msanii huyo anaacha kuimba injili alivunjika moyo sana.

Katika mahojiano na SPM Buzz, Syokau alisema kwamba taarifa za Ringtone kuondoka injili baada ya kuhubiri kwa muda mrefu zilimvunja moyo mpaka akaenda kanisani kufanya maombi ili msanii huyo atupilie mbali fikira na mawazo kama hayo ya kuhama injili na kuingia sekta ya sekula.

“Nilivunjika moyo sana mpaka nikaenda kituo cha maombi kumuombea Ringtone arudi kwa Yesu, kwa sababu ni mwenyekiti wa wasanii wa injili Kenya. Kwa hiyo nasema kwamba tuendelee kumuombea Ringtone amrudie Yesu kwa sababu alikuwa anaimba nyimbo nzuri,” Syokau alisema.

Alisema kwamba Ringtone aliimba kibao kimoja akimtaka msichana Pamela kurudi kwa Yesu lakini sasa wao ndio wanaimba Ringtone kurudi kwa Yesu.

Syokau alizidi kusema kwamba anataka Ringtone arudi kwa injili ili waonae.

“Unawezaje kutoka gospel kuliko uingie gospel tuonae, Bado namuombea Mungu amrudishe kwenye muziki wa injili. Jambo moja ninalopenda juu yake ni kwamba alikuwa na maudhui mazuri. Ringtone alikuwa akiimba kwa njia nzuri," Syokau alisema.

Mwaka jana, mwanamuziki huyo aliyejizolea umaarufu kutokana na kibao chake cha 2020 aligonga vichwa vya habari za udaku baada ya kusema kwamba alikuwa anataka Ringtone awe mpenzi wake na kusema kuwa katika muda mrefu alikuwa akimtolea macho Ringtone kutokana na fasheni yake kwenye mtandao wa Instagram.

Wasanii wa injili Ringtone na Justina Syokau
Wasanii wa injili Ringtone na Justina Syokau
Image: Instagram//Ringtone//JustinaSyokau2020