Dennis Karuri aonesha picha zake za kike na kiume "Pande mbili za sarafu"

Karuri ni mwanaume anayevalia na kujipodoa kama mwanamke.

Muhtasari

• "Mapenzi pacha, mwali pacha. Kubadilika kwa mtazamo. Kuzalisha uwezekano usio na kikomo,” Karuri aliandika.

Mwansaume anayewapodoa wasanii, Dennis Karuri
Mwansaume anayewapodoa wasanii, Dennis Karuri
Image: Instagram//DennisKaruri

Mwanaume anayevalia mavazi ya kike na kutumia mbinu hiyo kama njia moja ya kuendeleza biashara yake ya kuwapodoa wasanii, Dennis Karuri ameachia picha zake mbili katika pakio moja kwenye YouTube, zote zikionesha watu wawili tofauti kabisa kwa mtu ambaye ndio mara ya kwanza kumuona.

Karuri ambaye anajipodoa na kuwa mwanamke kabisa kwa muonekano alisema picha hizo mbili zinaonesha mtu mmoja kutoka pande zote mbili na kudokeza kwamba ana uwezo wa kufanya hivyo bila kusumbuka sana.

“Pande mbili za sarafu. Zote mbili za kweli bila taabu. Mimi ni Gemini. Machafuko mazuri kabisa. Mapenzi pacha, mwali pacha. Kubadilika kwa mtazamo. Kuzalisha uwezekano usio na kikomo,” Karuri aliandika.

Mwanaume huyo amekuwa kwa muda mrefu akishukiwa kuwa shoga kutokana na uvaaji wake wa kike huku pia akijimwayia marashi na kujipodoa sambamba na watoto wa kike.

Karuri si mwanaume wa kwanza kutoka na muonekano wa kike kwani nchini Kenya na utandawazi wa Instgram na Tiktok, wanaume wengi wapo radhi kuvalia kike ili tu kuendeleza mitikasi yao katika mitandao hiyo pendwa zaidi humu nchini.

Mchekeshaji Eric Omondi amekuwa wa hivi karibuni kutuhumiwa kuwa ni shoga kutokana na muoneka no wake ambao umewaacha Wakenya wengi kumsifia kwa jinsi alivyojivaa kama mwanamke kabisa kwa jina Divalicious huku akiongoza kipindi chake kipya kwenye mtandao wa YouTube.

Hawa wanajiunga katika orodha ndefu ya wanaume wanaovalia kama wanawake akiwemo Mtumba Man na Kelvin Kinuthia ambaye ndiye anasemekana kuwa mwanzilishi wa mtindo huo, wengi mpaka sasa wakishindwa kutambua jinsia yake halisi kutokana na muonekano wake wa kibonge kama mwanamke aliyejazia na kuwanda.