"Mimba imenifanya kuwachukia rafiki wa mume wangu" - Nandy

Nandy alisema kwamba mumewe anamuelewa kwa hilo na anajua ni mimba inasababisha.

Muhtasari

• Alimsifia Billnass kwamba licha ya kumuacha kwa miezi michache tu kiumri lakini kufikiria kwake ni kwa hali ya juu sana.

Wachumba Nandy na Billnass
Wachumba Nandy na Billnass
Image: Instagram//Nandy

Mwanamuziki Nandy usiku wa Alhamis alifunfuka makubwa katika mahojiano na mtangazaji maarufu Millard Ayo kuhusu ujauziro wake.

 Nandy alisema kwamba ujauzito ule umembadilishia tabia mpaka kutaja baadhi ikiwemo mimba ile kumtuma kuwachukia marafiki wa mume wake Billnass.

“Kuna tabia fulani ambazo wanawake wakiwa wajawazito wanakuwa nazo, yaani haukuwa nazo kabisa lakini ukiwa mjamzito unakuwa nazo, ni vitu gani ambavyo umeibukia kuvichukia?” Millard Ayo alimuuliza.

Nandy alijibu kwa kusema kwamba ni vitu vya ajabu sana kwani mojawapo ni kutowapenda rafiki wa mume wake.

“Wanajua na itabidi wanisamehe yaani wananiambia muda mwingine bana mimba yako haitupendi. Yaani akipiga simu rafiki wa mume wangu naeza nikaipokea mimi. Wakati mwingine anaeza nipigia simu aniambie ako na rafiki wangu na mimi kama niko na namba ya huyo rafiki yake naeza nikachukua simu na kumpigia kumwambia naomba asichelewe, akichelewa ni wewe,” Nandy alisema.

Nandy vile vile alisema kwamba kuna marashi ya kujipulizia ambayo alimnunulia Billnass yeye mwenyewe akitoka Nigeria lakini akaja kuyachukia marashi yale mwenyewe hali ya kuwa Billnass aliyakumbatia na kuyakubali. Alisema marashi yale yalikuwa ya bei ghali kweli.

Msanii huyo alisema vitu vingine ambavyo amejipata akivifanya kinyume na utaratibu wa awali kisa tu mimba ni pamoja na kumuansha mumewe usiku mkuu na kumtaka amtafutie vibanzi.

Nandy na Billnass walifunga ndoa ya kifahari wiki chache zilizopita baada ya kuvishana pete za uchumba Mwezi Februari.

Wanandoa hao wapya wanatikisa mitaa yote huku wakisubiria kujaaliwa na mtoto wao wa kwanza.

Katika baadhi ya maswali ambayo aligusia yaliyofurahisha wanamitandao, Nandy alimsifia mumewe kwa uelewa mkubwa na kusema kwamba Billnass amemzidi kwa miezi michache tu kiumri lakini kufikiria kwake ni kwa hali ya juu yaani mpaka anajivunia kuwa na mume kama huyo.