Paula afungua duka la nguo, asema ilikuwa ndoto yake kuwa CEO kwa umri mdogo

"Siwezi Kuongea Kuhusu Rayvanny Lakini Nina Boyfriend Kwa Sasa.....Tutajua Ijumaa" Paula

Muhtasari

• "Asante kwa mama yangu @kajalafrida. Umefanya safari yangu kuwa rahisi kuliko nilivyotarajia, Asante kwa kuwa hapo kila wakati nakupenda sana,” Paula alimtamkia mamake.

Mwanawe Kajala, Paula
Mwanawe Kajala, Paula
Image: Instagram//PaulaKajala

Ni hatua kubwa ya kibosi kwa mwanadada Paula Kajala ambaye ni mwanawe muigizaji mkongwe Kajala Masanja baada ya kufungua rasmi duka lake la kuuza nguo ambalo aliandaa tafrija ya kukata na shoka Ijumaa katika hafla ya kulifungua rasmi.

Paula alifurahia hatua hiyo kubwa katika maisha yake licha ya kuwa na umri mdogo na kusema kwamab hii ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu na hatimaye amefaulu kuitimiza.

“Wanawake, ninayofuraha kubwa kuwatangazia @paulahscloset imefunguliwa rasmi…Tuko tayari na tumejiandaa vyema kukuhudumia. Karibu usasishe kabati lako la nguo na upate mavazi maridadi kwa hafla yoyote ili ionekane maridadi, kuvutia, kurembeka na kung’ara zaidi,”

“Daima kuna kitu cha kushukuru katika maisha .... ilikuwa ndoto ya muda mrefu kwa msichana mdogo kama mimi kuwa Mkurugenzi Mtendaji mchanga wa ndoto zangu…. Nadhani nini. Hatimaye niliota ndoto hii ...” Paula Kajala aliandika kwa furaha.

Mwanadada huyo ambaye kwa muda fulani amesemekana kuwa nchini Uturuki kwa masomo alimshukuru mamake Frida Kajala kwa kusimama naye pamoja pia na kuwashukuru wengine waliosimama naye katika safari ya kufanikisha ndoto zake.

“Asante kwa kila mtu aliyeniunga mkono, aliyechangia na kufanikisha ndoto hii… Asante kwa mama yangu @kajalafrida. Umefanya safari yangu kuwa rahisi kuliko nilivyotarajia, Asante kwa kuwa hapo kila wakati nakupenda sana,” Paula alimtamkia mamake.

Paula pia alidokeza kuwa na mchumba mwingine alipoulizwa kuhusu mchumba wake wa zamani Rayvanny, alikataa kumzungumzia na kusema kwamba ana mpenzi mwingine.

"Siwezi Kuongea Kuhusu Rayvanny Lakini Nina Boyfriend Kwa Sasa.....Tutajua Ijumaa" Paula Kajala alisema huku akiwaambia wakuza maudhui waliotaka kujua ni nini hicho alichokuwa akiwaambia Ijumaa.