Amber Ray Amshauri Jimal Kuwa Mkweli na Kurudi Kuijenga Familia Yake

Alisema hana tatizo na aliyekuwa mke wa kwanza wa Jimal, Amira.

Muhtasari

• Amber Ray alikuwa anajibu maswali ya mashabiki wake kweney Instagram kipindi cha maswali na majibu.

Mwanamitindo Amber Ray
Mwanamitindo Amber Ray
Image: Instagram//Amber Ray

Mwanasosholaiti Amber Ray ambaye alikuwa mke wa pili wa mfanyibiashara Jimal Rohosafi sasa anamshauri mwanaume huyo kujifikiria maracmbili na kurudi nyumbani kuikarabati familia yake.

Ray ambaye asubuhi ya Jumatano alikuwa anazungumza na mashabiki wake katika kipengele cha maswali na majibu kwenye instastories zake alijibu shabiki mmoja ambaye alimuuliza kama kweli anajifanya haoni jinsi Jimal anazidi kusononeka na kuteseka kwa kukosa mapenzi ambapo kwa mikumbo kadhaa ameonekana hadharani akiomba radhi kwa mke wake wa kwanza Amira akimtaka kumkubali kurudiana kwa ahadi kwamba amebadilika pakubwa kitabia na kwamba anajutia makosa yake ya awali yaliyosababisha msambaratiko wa ndoa yao ya miaka mingi.

“Mbona unajifanya kama huoni Jimal anateseka kwa kukosa mapenzi, kwani ulimpa nini?” Shabiki mmoja alimuuliza.

“Anafaa kuwa mkweli kwa nafsi yake na pengine kujirudi na kuangazia kuikarabati familia yake,” alijibu Amber Ray.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa tofauti kati yake na aliyekuwa mke mwenza, Amira na kama wanaweza kurudi waketi chini kama watu wazima ili kusuluhisha tofauti hizo, Amber Ray alijitetea vikali akisema kwamba yeye hana tatizo na kwamba Amira ndiye alikuwa anamuonea tu bila sababu.

“Mbona msisuluhishe tofauti zenu na Amira, mwanamke anafaa kumsapoti mwanamke mwenziwe,” shabiki alimuuliza.

“Mii sina tatizo na yeye, shinda ilikuwa kwamba alikuwa ananiwekelea kila kitu akijua vizuri kwamba shida haikuwa mimi. Ila sasa anatumai amegundua tatizo halikuwa mimi,” Amber Ray alijibu.