Picha ya Siku: Mke wa Seneta Mutula Kilonzo Akimuangalia Kwa Mahaba

“Napenda hivi. Mwanamke anakutamani bila kuficha. Ni tamu unapoitambua baadaye,” mmoja alisema.

Muhtasari

• Kilonzo Junior ni wakili wa mahakama ya juu ambaye aliteuliwa kwa mara ya kwanza kama seneta wa Makueni mnamo Julai 2013.

• “Napenda hivi. Mwanamke anakutamani bila kuficha. Ni tamu unapoitambua baadaye,” mwingine kwa jina Mwalimu Kimathi alidokeza.

Mutula Kilonzo Junior na mkewe Anita Mutula
Mutula Kilonzo Junior na mkewe Anita Mutula
Image: Twitter//AnitaMutula

Picha ya mkewe seneta wa Makueni Mutula Kilonzo Junior, Anita Mutula akimtazama mumewe kwa macho ya mahaba huku akiwa ameuma midomo kwa tabasamu kubwa imepasua mitandao ya kijamii kwa furaah kubwa.

Picha hiyo iliyopakiwa kwenye mtandao wa Twitter Jumanne siku ya uchaguzi mkuu inawaonesha wanadnoa hao wawili wakiwa wanazungumza na wanahabari pindi tu baada ya kupiga kura na wakati Kilonzo Junior alikuwa anazungumza, mkewe Anita Mutula alinaswa na kamera akiwa amemtazama mumewe kwa furaha na tabasamu la kimahaba, jambo ambalo limezungumziwa sana kwenye mitandao ya kijamii.

“Wadau baada ya uchaguzi tusisahau kuzungumzia picha hii nzuri,” mmoja kwa jina Brian Korir alisema.

“Napenda hivi. Mwanamke anakutamani bila kuficha. Ni tamu unapoitambua baadaye,” mwingine kwa jina Mwalimu Kimathi alidokeza.

Wanandoa hao kwa muda mrefu hawajakuwa wachoyo katika kuwapa wanamitandao kile wanachotaka kwani huoneshana mapenzi yao mubashara kwenye mitandao ya kijamii huku seneta huyo akimmiminia sifa mkewe pamoja na watoto wao ambao huwapakia mara kwqa mara kweney kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Mutula Kilonzo Junior alikuwa anawania kama gavana kumrithi gavana anayeondoka Kivutha Kibwana ambaye kama vile wanabadilishana huku yeye akiwania useneta safari hii baada ya kumalizika kwa kipindi chake cha miaka 10 kulingana na katiba ya Kenya.

Kilonzo Junior ni wakili wa mahakama ya juu ambaye aliteuliwa kwa mara ya kwanza kama seneta wa Makueni mnamo Julai 2013 miezi michache tu baada ya kifo cha babake Mutula Kilonzo ambayealiteuliwa kweney uchaguzi wa Machi mwaka huo baada ya kuhudumu kama Waziri wa elimu.