Picha Ya Siku: Ruffton Apiga Magoti Kuchukua Picha na Wanadada Mbilikimo

Ruffton alikuwa na azma ya kuwania useneta Nairobi wa tikiti ya UDA kabla ya kughairi.

Muhtasari

• Mashabiki wake walimsherehekea kwa kuonesha unyenyekevu wa kuenda chini magotini ili tu kufikia kimo cha wanadada hao kwa ajili ya picha ya pamoja.

Msanii mkongwe wa injili, Ruffton
Msanii mkongwe wa injili, Ruffton
Image: Ruffton//Instagram

Mwanamuziki mkongwe wa injili Ruffton ameshabikiwa na watu wengi kwenye mtandao wa Instagram baada ya kupakia picha ya pamoja akiwa na wanawake wafupi katika picha ya pamoja.

Kilichofurahisha wengi ni kwa jinsi mwinjilisti huyo alionesha ishara ya unyenyekevu kwa kipiga magoti chini ii kuweza kufikia kimo cha mbilikimo hao kwa sababu ya picha ya pamoja.

Ruffton alikuwa katika kituo kikuu cha kuhesabia kura cha Bomas jijini Nairobi kushuhudia mchakato huo ambao unafuatiliwa na idadi kubwa ya wakenya siku tatu tangu uchaguzi mkuu ulipofanyika na hapo ndipo alikutana na wanadada hao watatu mbilikimo na kuchukua picha nao.

Nchini watu wafupi kwa muda mrefu wamekuwa wakisemekana kujihisi kudharauliwa na watu wamrefu na kitendo cha Ruffton kujinyenyekesha kwa kupoga magoti sakafuni kwa ajili ya picha nao kilishabikiwa kama ishara ya kuwaonesha watu wafupi upendo.

“Hiyo ni nzuri.watu wafupi pia ni wanadamu, wameumbwa kwa uzuri sana na wa ajabu na Mungu,” mmoja alimwambia.

Ruffton awali alikuwa ametangaza azma yake ya kuwania useneta katika kaunti ya Nairobi kutumia tikiti ya chama cha UDA na ila baada ya mashauriano ya muda na viongozi wa chama aliamua kuiweka akiba azma yake hiyo na kumuunga mkono Askofu Margret Wanjiru ambaye chama kiliafikiana kwamba anafaa na kumkabidhi tikiti.

Wanjiru anamenyana na katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna ambaye anagombea useneta Nairobi kwa tikiti ya chama hicho.