Willy Paul amsherehekea Mbunge Oluoch kwa Kumbwaga Bahati "Watu ni wewe wanahitaji!"

Katika ujumbe ambao Willy Paul alindikia Oluoch, wengi waliutafsiri kama njia moja ya kumtupia bomu Bahati

Muhtasari

• "MATHARE ndio nyumbani kwangu na ninafuraha kuwa iko kwenye mikono Salama tena,” Willy Paul aliandika

Wasanii Bahati Kioko na Willy Paul
Wasanii Bahati Kioko na Willy Paul
Image: Instagram

Mwanamuziki Willy Paul ameendeleza uhamasa wake dhidi ya mwanasiasa mwenza Bahati Kioko.

Hii ni baada ya Willy Paul kuandika wazi kweney mitandao yake ya kijamii kumhongera kwa maneno matamu mbunge mteule wa Mathare, Anthony Oluoch wa ODM ambaye alikuwa mshindani mkubwa wa Bahati Kioko aliyewania kupitia chama cha Jubilee na kushindwa.

Katika ujumbe ambao Willy Paul alindikia Oluoch, wengi waliutafsiri kama njia moja ya kumtupia bomu Bahati na kumcheka kwa kupoteza katika uchaguzi huo.

“Hongera Antony Oluoch kwa Kushinda KITI CHA UBUNGE MATHARE. Wewe ndio watu wa MATHARE wanahitaji bwana. Hakika umefanya kazi nzuri mheshimiwa, kubaki na hicho kiti si rahisi! Endelea kusukuma, MATHARE ndio nyumbani kwangu na ninafuraha kuwa iko kwenye mikono Salama tena,” Willy Paul aliandika.

Wengi walikuwa wanatarajia Bahati angechaguliwa kama mbunge ila mshangao mkubwa ukawagubika baada ya matokeo kubaini kwamba alibwagwa hadi nafasi ya tatu nyuma ya mgombea wa ODM Anthony Oluoch na Billian Ojiwa wa UDA aliyemaliza wa pili.

Awali, rafiki wa karibu msanii wa Bahati, DK Kwenye Beat alimliwaza kwa kushindwa na kumhimiza kwamba ipo tena nafasi ya kujaribu katika uchaguzi mwingine ujao.

Katika safari yake ya kuwania kuwa mbunge wa Mathare, Bahati alikumbwa na vizingiti si haba kutoka kwa baadhi ya viongozi wa muungano pana wa Azimio la Umoja One Kenya ambapo mara kadhaa walimtaka akaghairi azma yake ya kuwa mbunge na badala yake kumuunga mkono Oluoch ila mwanasiasa huyo akakaidi kabisa.

Bahati na Willy Paul kwa muda mrefu wamekuwa na uhasama kimuziki tangu walipokuwa katika sekta ya miziki ya injili na mpaka kuingia kwao katika miziki ya sekula ambapo kila mmoja anajaribu kuudhirishia umma ubabe wake katika kutunga miziki mizuri yeney mvuto.