“Sisi wengine hubebwa kwa maombi" Jemutai alipoona Hamo na mwanamke mgongoni

Jemutai na Hamo waliweka wazi kwamba wanaishi na kulea watoto wao pamoja licha ya tofauti za awali.

Muhtasari

• “Sisi wengine hubebwa kwa maombi. Ati kama ni wako atarudi kwani mapenzi ni stima,” Jemutai aliandika kwenye Instagram yake.

Wachumba
Wacheshi Jemutai na Hamo Professor Wachumba
Image: INSTAGRAM//JEMUTAI

Baada ya picha ya mchekeshaji Hamo Professor kuonekana akiwa amebeba mwakamke mwingine mwenye umbo la kadri mgongoni, mzazi mwenziwe ambaye pia ni mchekeshaji Jemutai ametolea neno lake katika picha hiyo ambayo imewasha bashasha mitandaoni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jemutai alipakia picha hiyo na kudai kwamba yeye hajawahi bebwa hivyo na pengine anabebwa tu hivyo katika maombi pekee.

“Sisi wengine hubebwa kwa maombi. Ati kama ni wako atarudi kwani mapenzi ni stima,” Jemutai aliandika kwenye Instagram yake.

Miaka miwili iliyopita Hamo alijipata katika zogo la kumchafulia jina pakubwa baada ya mchekeshaji mwenza, Jemutai kumtuhumu hadharani kwamba wana watoto wawili pamoja lakini amewatelekeza licha ya Hamo kipindi hicho kuwa na kazi kama mtangazaji kwenye kituo kimoja cha redio nchini.

Sakata hilo lilitokota hata zaidi mpaka kuwapelekea wawili hao kuelekea hospitalini kutafuta huduma za msumbojeni yaani DNA ili kutambua kama kweli Hamo alikuwa baba mzazi na matokeo yakamuonesha kuwa baba wa kuwazaa watoto wale.

Hilo lilimdhalilisha sana moaka kuachishwa kazi katika redio ambapo muda mchache baadae alimuomba Jemutai msamaha hadharani na kuahidi kushirikiana kulea watoto wao pamoja licha ya kuwa na mke mwingine ambaye alikuwa anajulikana kihalali.

Pia wiki kadhaa zilizopita wachumba hao wawili waliletana juu katika video moja Instagram ambapo Hamo alikuwa na mpango wa kutaka kuruhusiwa kutafuta nyumba yake kando na kuishi kivyake ili kujivinjari katika maisha, jambo ambalo Jemutai alilipinga vikali na kusema kwamba mawazo na fikira kama hizo ni za usherati.