"Ukitaka kujua kama mpenzi wako anakusaliti, mnuse!" - Mtangazaji Gateere

Alisema yeye hakuwahi kusalitiwa katika penzi lake ya awali.

Muhtasari

• "Najua unajua jinsi harufu ya mtu wako ilivyo, ukimnusa kama anachepuka utajua tu juu wanaanza kutoa harufu tofauti,” Gateere

Mtangazaji Karigoh Gateere akisauri mbinu ya kujua kama mpenzi wako anakusaliti kimapenzi
Mtangazaji Karigoh Gateere akisauri mbinu ya kujua kama mpenzi wako anakusaliti kimapenzi
Image: Instagram

Mtangazaji wa zamu katika kituo kimoja cha redio cha humu nchini Karigoh Gateere amekuja na ushauri kuhusu mbinu mpya ya kutumia ili kujua kama mpenzi wako anakusaliti katika mapenzi kwa kuchepuka au la.

Mtangazaji huyo anayefanya kipindi cha kuzungumzia masuala ya watu wazima muda mwingi amewaambia wachumba kwamba ni rahisi sana kujua mwenzako kama ameanza tabia ya kudoea mapenzi nje na mbinu hiyo ni kwa kumnusa tu.

Katika kutetea mbinu yake, Gateere amewaambia mashabiki wake kwamba kwa kawaida kama umekaa na mtu kwenye mahusiano kwa muda, bila shaka utakuwa unajua jinsi harufu yake iko na kama ameanza kuchepuka utajua tu kwa sababu harufu yake itabadilika ghafla.

Katika video ambayo aliipakia kwenye Instagram yake mwishoni mwa wiki, Gateere alisema kwamab hiyo mbinu imekuwa ikifanya kazi kwake vilivyo na hata katika mahusiano yake ya awali hakuwahi kusalitiwa kwa milupo na michepuko hata kidogo.

“Ishara na dalili za mtu anayekusaliti, mnuse. Najua unajua jinsi harufu ya mtu wako ilivyo, ukimnusa kama anachepuka utajua tu juu wanaanza kutoa harufu tofauti,” Gateere alisema.

"Ikiwa unashuku kuwa mpenzi wako anadanganya labda ndivyo, mimi hulala vizuri zaidi usiku kwa sababu sijaoa na hakuna anayenidanganya." aliongeza.