Vanessa Mdee ateta kwa kutolipwa pesa zake na kampuni ya kusambaza miziki

Alisema kampuni hiyo imemkwamia kumjibu hata baada ya kutumia njia ya kitaalamu.

Muhtasari

• "Mziiki nawaomba mnilipe pesa zangu kwa makubaliano tuliyo nayo. Nimejaribu kufuata njia ya kitaaluma na timu yangu sasa imefikia hatua ya nyinyi kutokujibu,” Mdee alilalama vikali.

• Baadae kampuni hiyo ilimjibu na kusuluhisha tatizo lao.

Aliyekuwa mwanamuziki Vanessa Mdee ateta kutolipwa pesa zake za muziki
Aliyekuwa mwanamuziki Vanessa Mdee ateta kutolipwa pesa zake za muziki
Image: Instagram

Aliyekuwa mtangazaji na mwanamuziki wa Bongo Fleva Vanessa Mdee wiki iliyopita aliwajia juu mtandao wa kupakia na kuuza muziki duniani "MZIIKI" kwa kutomlipa mapato kutokana na kazi zake za mziki kwa muda mrefu.

Mdee aliandika hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter huku akibainisha kuwa wasanii wamekuwa wakifanya kazi kubwa sana kuja na ubunifu ambao wanauweka kwenye kazi zao lakini hawapati kile wanachostahili.

Ikumbukwe kuwa Vanessa Mdee alitangaza kuacha muziki mnamo mwezi juni mwaka 2020 akieleza msongo wa mawazo katika muziki ndio uliopelekea yeye kujiengua katika tasnia hiyo.

“Jamani pesa za muziki zinatafutwa kwa shida kweli kweli na wasanii kuanzia kubuni hadi kufikia kwa wananchi. Mziiki nawaomba mnilipe pesa zangu kwa makubaliano tuliyo nayo. Nimejaribu kufuata njia ya kitaaluma na timu yangu sasa imefikia hatua ya nyinyi kutokujibu,” Mdee alilalama vikali kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Katika kile kilionekana kama kampuni hiyo ilimjibu na pengine kumuahidi mazuru kuhusu malimbikizi yake, Mdee aliufuta ujumbe wa awali na kuwashukuru wailiki wa Mziiki kwa kumjibu kwa ufasaha.

“Asante @Mziiki kwa kujibu na kuturudia baada ya kutweet nawashukuru wanaTwitter. Haihitaji kuwa hivi,” Mdee aliandika kwenye tweet nyingine ishara kwanga waliyasluhisha na kampuni hiyo.

Awali alikuwa amewataka wasanii wote wanaoidai kampuni hiyo malimbikizi yao kujimwaga kwenye ujumbe huo wake ili kuwataja mpaka wasikie kilio chao na kuwalipa pesa zao zinazotokana na kusambaza kazi zao za miziki.