Mama Margret Kenyatta ni mamangu wa pili - DJ wa ikulu Euphorique Ignatius

Alipakia picha nzuri ya pamoja na mama wa taifa na kuwatakia wakenya wikendi njema

Muhtasari

• “Kutoka kwa mama yangu wa pili H.E Mama Margret Kenyatta na mimi tunawatakia wikendi njema mbeleni,” Mcheza santuri huyo aiandika.

Mcheza santuri rasmi wa ikulu amemshukuru mama wa taifa na kumuita mamake wa pili.
Mcheza santuri rasmi wa ikulu amemshukuru mama wa taifa na kumuita mamake wa pili.
Image: INSTAGRAM

Mcheza santuri wa ikulu DJ Euphorique ambaye ni mlemavu amepakia picha ya hivi punde na mama wa taifa mkewe rais anayeondoka Uhuru Kenyatta, Margret Kenyatta na kumsifia pakubwa.

Katika picha hiyo alipopakia Instagram yake, DJ huyo mwenye ulemavu wa miguu ambapo anasaidia kusonga kutoka sehemu moja kuelekea nyingine kwa kutumia kiti cha magurudumu amemsifia maam wa taifa na kumuita kama mama yake wa pili katika uso wa dunia.

“Kutoka kwa mama yangu wa pili H.E Mama Margret Kenyatta na mimi tunawatakia wikendi njema mbeleni,” Mcheza santuri huyo aliyebarikiwa na uwezo wa kufanay mambo kwa njia tofuauti kabisa alisema.

Rais Kenyatta alimuunga mcheza santuri huyo kama moja ya waburudishaji wa ikulu pamoja na kwaya rasmi ya ikulu ya Nairobi mwaka 2017.

Katika mahojiano ya awali, Euphorique alielezea jinsi alivyojipata ikulu akitumbuiza rais na wageni wake.

“Nilipoanza mwaka wa 2017, ilikuwa kama mzaha. Nilipigiwa simu na Ikulu na mtu fulani akasema nilihitajika kucheza wakati wa hafla. Sikujua kuwa mimi ndiye deejay pekee niliyealikwa pale, achana na mawazo kuwa naenda kumtumbuiza raisi. Hiyo ndiyo siku ya kwanza kukutana na Uhuru,” mcheza santuri huyo alinukuliwa katika mahojiano ya awali.

Mcheza santuri huyo alipata umaarufu wake mwaka 2016 wakati ambapo washikadau katika sekta ya Sanaa nchini waliungana mikono na kuchangisha pesa za kumnunulia mashine ya kucheza miziki kabla ya ikulu kuona jitihada zake na kumpa kazi kama mtumbuizaji rasmi wa rais.