"Mlisema mtegemea cha ndugu hufa maskini" Kakake Diamond ajibu kejeli za kutangaza uganga

Romy Jons alikejeliwa dhidi ya kufanya matangazo ya biashara za waganga wa kienyeji licha ya kakake kumiliki helikopta.

Muhtasari

• "Mbona mnanichanganya sasa?” Romy Jons aliandika kwa uchungu mwingi.

Romy Jons ashindwa kuwaelewa wanamitandao wanaomsuta kila upande kisa utajiri wa nduguye mdogo, Diamond Platnumz.
Romy Jons ashindwa kuwaelewa wanamitandao wanaomsuta kila upande kisa utajiri wa nduguye mdogo, Diamond Platnumz.
Image: instagram

Juzi kati kumeibuka na maoni fulani kwenye mtandao wa Instagram ambayo yamezungumziwa sana ya mtu mmoja akimkandia na kumsimanga vikali nduguye mkubwa wa Diamond Platnumz, Rommy Jones ambaye pia anajiongeza kama mcheza santuri rasmi wa Mond.

Katika maoni hayo, shabiki mmoja anamjia juu Jons kwa kumwambia kwamba yeye anajishughulisha na biashara hovyo ya kupakia matangazo ya waganga wa kienyeji kwa malipo duni ilhali ndugu yake mdogo ambaye ni Diamond ametoka nyuma na kumiliki ndege aina ya helikopta na kwa sasa ananukia utajiri mno.

Kwa kuweka mambo wazi, mdau huyo hajakosea kusema kwamba Jons anafanya matangazo ya waganga wa kienyeji kwani ndio ukweli mtupu huo ila alichokisahau ni kwamba hayo matangazo si bure kwani pia analipwa na ndio moja ya njia yake Jons kupata posho lake kando na kuwa DJ wa Diamond.

“Mdogo wako ananunua ndege na wewe uko hapo unapakia matangazo ya waganga wa kienyeji ili ulipwe elfu 20 za Tanzania. Maisha hata hayana usawa,” Jamaa huyo anamzingua Jons kwenye Instagram.

Maoni haya yalimpata Jons kwa mshtuko ambapo ilimlazimu kujibu kwa uchungu huku akidokeza kwamab mashabiki wengine hawaridhiki na wanamchanganya kwani hao hao ndio walimuambia kwa kipindi kimoja kwamba ajitegemee na kuacha kutegemea vya nduguye.

“Jamani si mmeniambia nisitegemee cha ndugu kuwa nitakufa maskini, mbona mnanichanganya sasa?” Romy Jons aliandika kwa uchungu mwingi.

Wengine walimsuta Jons kwamba anamharibia jina ndugu yake kwa kukubali matangazo ya uganga na kuongeza shepu za mwili kwani yeye tayari kwa kuwa ndugu yake amelijenga jina basi naye moja kwa moja yumo pale na hafai kukubali matangazo ya chini kama hayo.

Kwel hata Mimi sipendi matangazo yako ya kipuuzi liko la waganga na za kuongeza Shepu; hata kama unapata hela matangazo Kama hayo wafanyage wasanii wadogo. Yaani ulivyo na matangazo ya waganga hamuendani, badilika bhana,” shabiki kwa jina la Deborah alimwambia kweney Instagram yake baada ya kupakia majibizano hayo na shabiki.