Ommy Dimpoz kupakiwa ukurasa wa Instagram wa Man-U alitumia uchawi - Mwijaku

Imekuwa ni kawaida sana kwa Wabongo kutuhumu wenzao wamejiunga kwenye Ufreemason mara baada ya Mafanikio ya ghafl

Muhtasari

"Haiwezekani ..! Jamani kuna siri gani hapa ? @ommydimpoz huyu huyu au kuna TAJIRI nyuma yake ? Natamani nimjue ..!" Mwijaku alilia.

Mtangazaji mwenye utata Mwijaku amesema kwamba Ommy Dimpoz alitumia nguvu za giza ili kutambuliwa na Manchester United mpaka kupakiwa.
Mtangazaji mwenye utata Mwijaku amesema kwamba Ommy Dimpoz alitumia nguvu za giza ili kutambuliwa na Manchester United mpaka kupakiwa.
Image: Instagram

Msanii Ommy Dimpoz kutoka Tanzania yupo nchini Uingereza kwa muda yapata wiki moja sasa kwa mwaliko rasmi wa timu ya soka ya Manchester United na amekuwa akipakia picha na wachezaji mbali mbali wakiwepo wa timu hiyo na wale wa Liverpool baada ya kukutana nao katika mechi ya ligi kuu Jumatatu usiku.

Ila tukio kubwa ambalo limezungumziwa sana ni baada ya ukurasa rasmi wa Instagram wa timu ya Manchester United kuipakia picha ya Ommy kwenye instastories zake na hili limekuwa gumzo haswa nchini Tanzania, baadhi wakisema kwamba msanii huyo ametumia ulozi kujipata katika kiwango hicho ambacho sasa ametambuliwa na ulimwengu mzima wa mashabiki wapatao milioni 59.9 wanaoshabikia timu hiyo kwenye Instagram.

 

Mmoja wa watu ambao wametilia shaka usuhuba kati ya Ommy na Manchester ni mtangazaji mwenye utata nchini Tanzania, Mwijaku ambaye ameibuka na suala la ushirikina ambao Watanzania wengi wanaliita "U-freemason" na kusema kwamab haiwezekani kwa Ommy kukwea mpaka kujipata kwenye ukurasa wa timu kubwa hivo pasi na jambo la ulozi ambalo limetumika.

"Kuna siri gani kati ya Man united na @ommydimpoz. Mpaka kwenye ukurasa wao jamani ? Au freemason ? Haiwezekani" aliandika Mwijaku katika ukurasa wake wa Twitter.

 

Mtangazaji huyo pia alizidi kukanusha ukweli na uhalisia huo wa Ommy kupakiwa kwenye Instagram ya Manchester United na kuzidi kulalama kupitia kurasa mbali mbali za mitandao yake ya kijamii akisema kwamba huenda kama si ushirikina basi kuna Tajiri mwenye ushawishi mkubwa sana nyuma ya ziara ya Ommy kule katika jiji la Manchester.

"Haiwezekani ..! Jamani kuna siri gani hapa ? @ommydimpoz huyu huyu au kuna TAJIRI nyuma yake ? Natamani nimjue ..!" Mwijaku alilia.

Imekuwa ni kawaida sana kwa Wabongo kutuhumu wenzao wamejiunga kwenye Ufreemason mara baada ya Mafanikio ya ghafla, hivyo sio ajabu kabisa Mwijaku kumtuhumu Ommy Dimpoz.

Mpaka sasa inadaiwa kuwa Ommy Dimpoz ndio mtanzania wa Kwanza Kupiga picha na Cristiano Ronaldo pia ndio Mtanzania wa kwanza kupostiwa kwenye Page ya Manchester United.