Ommy Dimpoz - Sijaoga tangu Christiano Ronaldo anishike bega

"Yaani sijaoga tangu amenishika bega" - Ommy Dimpoz alisema.

Muhtasari

• "Yaani sijaoga tangu amenishika bega" - Ommy Dimpoz alisema.

Msanii wa Bongo Fleva pichani na mshambuliaji wa Ureno, Christiano Ronaldo
OMMY DIMPOZ Msanii wa Bongo Fleva pichani na mshambuliaji wa Ureno, Christiano Ronaldo
Image: instagram//ommydimpoz

Msanii wa muda mrefu wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz sasa ameibuka na madai mengine mapya kabisa akidai kwamba wiki moja na ushee hivi tangu fowadi wa Machester United, Christiano Ronaldo kumshika bega, hajawaho koga.

Kupitia instastories zake, Ommy Dimpoz alifichua haya kwa kupakia picha ya jarida moja ambalo lilimuangazia na ziara yake Old Trafford alikokuwa Jumatatu wiki jana kuhudhuria mubashara mtanange kati ya United na Liverpool. Mchezo huo ulikamilika kwa United kujivunia ushindi wa kwanza wa msimu baada ya kupoteza michezo miwili ya utangulizi kwenye ligi kuu ya Uingereza, EPL.

Akiwa ugani Old Trafford, Dimpoz alipata nafasi aula ya kupiga picha na baadhi ya mastaa tajika kutoka pande zote mbili zilizokuwa zikitifuana.

Alitajwa kuwa Mtanzania wa kwanza kuwahi kutokea ambaye alipiga picha na mchezaji nguli Christiano Ronaldo, jamaa ambaye jina lake limekuwa kama kaya kwenye tasnia ya soka, na kuwa mwanadamu mweye ufuasi mkubwa zaidi mtandao wa Instagram.

Baada ya jarida hilo kuangazia hadithi yake na kuipa kichwa kwamba Christiano amezidi kumpa Dimpoz kiburi kutokana na kujishaua ambako ameendeleza mitandaoni, msanii huyo alikwenda pale na kusema mikogo yake itazidi kwani hata kuoga bado hajawazia tangu Ronaldo kumgusisha bega, hii ikiwa ni wiki na siku kadhaa juu sasa.

Ommy Dimpoz amekuwa mkimya kwenye muziki kwa miaka kadhaa sasa ila kitendo cha yeye kupiga picha na Ronaldo kilimfanya kuzungumziwa ndani na nje ya Tanzania.

Dimpoz pia aliingia kwenye rekodi za historia kwa kuwa mtu wa kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kuwahi kupakiwa kwenye instastories ya timu ya Manchester United, ukurasa ambao una wafusi wapatao milioni 59.9 kutoka pembe zote za dunia. 

Jambo hilo liliwafanya wabwatukaji kama mtangazaji Mwijaku kuzua mjadala mwingine kwamba Dimpoz kupata umaarufu katika ukurasa wa timu kubwa kama ile kutakuwa si bure. Alisema kutakuwa kama si mkono wa tajiri mwekezaji basi ni ushirikina, Wabongo wanautaja kuwa Freemason.