Wahu na Nameless ni wanandoa wa muda mrefu ambao wameshabikiwa pakubwa na Watu wengi ndani na nje ya Kenya.

"Nitaenda popote na wewe, lakini kuingia leba siwezi" - Nameless amwambia Wahu

Wawili hao walikuwa wakizungumza katika mkutano mubashara Facebook.

Muhtasari

• Nameless alisema sababu ya kutoingia kwenye leba na yeye ni kuogopa kuvutwa nywele na Wahu kama ambavyo alimfanyia katika mimba ya awali.

• Wahu alimwambia alimvuta nywele kwa sababu alikuwa amekwama kwenye simu huku yeye akiungulia uchungu wa kutotoa.

Wanandoa hao wanatarajia mtoto wao wa tatu hivi karibuni
Wahu, Nameless Wanandoa hao wanatarajia mtoto wao wa tatu hivi karibuni
Image: Instagram

Wanandoa Nameless na Wahu usiku wa kuamkia Alhamis walikuwa na kipindi cha moja kwa moja kwenye mitandao yao ya Facebook ambapo walikuwa wanazungumzia mabo tofauti tofauti.

Wahu alikuwa akizungumza kutoka Kenya huku mumewe Nameless akizungumza naye kutoka Marekani ambapo amekaa zaidi ya wiki sita akifanya ziara ya muziki wake.

Moja ya suala ambalo wawili hao walizungumzia ni kuhusu ujauzito wa Wahu. Ujauzito ambao waiuweka waziwiki moja tu kabla ya Nameless kuondoka kuelekea Marekani.

Nameless anatarajiwa kurejea nchini Wiki hii baada ya kumalizika kwa ziara yake na Facebook walikuwa wanazungumzia mambo mbali mbali katika safari yao ya mapenzi, haswa kukumbushana kuhusu picha kadhaa ambazo Nameless alizipakia wakiwa Marekani mwaka 2004 na mkewe.

Nameless alimwambia mkewe Wahu kwamba hata kama anarejea nchini wiki hii lakini kuna baadhi ya vitu hatashiriki na yeye.

Alisema kwamba ashaongeza uzito na kumuahidi kufanya kila kitu na yeye ila akamwambia kwamba jambo ambalo hatoshiriki na yeye ni kuandamana na yeye kuelekea chumba cha kina mama kujifungua.

“Nitashiriki pamoja nawe katika kila kitu. Lakini kitu kimoja ambacho nitaweka mipaka ni kuenda na wewe leba kwa vile unapenda kuvuta nywele zangu. Mimba ya pili, nilihakikisha kuwa niko mbali,” Nameless alimtania mkewe.

Hapo ndipo mkewe alijibu mipigo kwa kuzungumzia kitendo hicho cha kumvuta nywele mumewe wakati wa kujifungua mtoto wa kwanza.

Wahu alisema kwamba alifanya kuvuta nywele zake kama njia moja ya kujituliza kutoka uchungu wa kuzaa kwani alikuwa akihangaika ilhali mumewe Nameless alikuwa amekita macho yake kwenye simu.

Aliongeza kwa kusema kwamba wanaume wengi hawangeweza kuhimili uchungu wa kuzaa mwana kama majukumu hayo yangebadilishiwa katika kila jinsia.

“Niko kwenye uchungu na wewe uko kwenye simu. Unakumbuka? inakuwaje hata hivyo? Nadhani wanaume wengi hawawezi kuhimili kazi ikiwa majukumu yanaweza kubadilishwa. Idadi ya mara ninazougua na hakuna anayejua ni nyingi sana kwa upande mwingine, wakati Nameless anapata mafua, kila mtu lazima ajue kuihusu,” Wahu alirusha mchanga kweney udhaifu wa jinsia ya kiume.