Baraka the Prince amkana Alikiba, aingia orodha ya Harmonize dhidi ya Diamond

Baraka the Prince alikuwa chini ya Kings Music lebo inayoongozwa na Alikiba.

Muhtasari

• Baraka the Prince alikuwa akitumbuiza ambapo alikataa kuimba collabo yake na Alikiba.

Msanii Baraka amemkana Alikiba,
Baraka the Prince, Alikiba Msanii Baraka amemkana Alikiba,
Image: Instagram

Msanii Baraka the Prince ameingia tena kwenye mzozo wa mitandaoni na mashabiki wa staa wa bongo fleva Alikiba kwa kile alisema kwamba hampendi hata kidogo bosi huyo wake wa zamani.

Mwishoni mwa wiki jana, Baraka alikuwa akitumbuiza Mwanza ambapo alikiri hadharani jukwaani kwamba hampendi Alikiba.

Hii ni baada ya mashabiki kumtaka kutumbuiza kibao ambacho walishirikiana na Alikiba miaka mitano iliyopita wakati alikuwa chini ya rekodi lebel ya Kings Music inayoongozwa na Alikiba.

“Mimi simpendi Alikiba, simkubali ndio maana sijataka kuimba wimbo niliofanya na yeye,” Baraka the Prince alimwambia mwanablogu wa YouTube.

Msanii huyu anaingia kwenye orodha ya mastaa wa muziki katika ukanda wa Afrika mashariki ambao wametofautiana na mabosi wao waliokuwa wamewaandikisha mkataba katika lebo za muziki.

Wasanii wengine ambao waliingia kwenye vita vya maneno na mabosi wao ni pamoja na;

Harmonize na Diamond

Kiongozi huyo wa lebo ya Konde Music Worldwide aliipata umaarufu katika muziki baada ya kushikwa mkono na Diamond ambaye alimpa mkataba mnono katika lebo yake ya Wasafi.

Ila baada ya miaka michache Diamond na Harmonize walivurugana jambo lililopelekea Harmonize kuondoka na kuanzisha lebo yake ya Konde huku akiibua shtuma na madai mengi dhidi ya Diamond. Moja ya madai ambayo aliyaibua ni kuwa alikuwa akinyonywa mtaji wa kazi zake za muziki chini ya Wasafi kwa kile alisema kwamba alikuwa anavuna 40% tu huku asilimia iliyosalia ikienda kwa lebo.

Bahati na Peter Blessing, Weezdom, David Wonder

Msanii Bahati kwa wakati mmoja alikuwa mmiliki wa lebo kwa jina EMB ambayo ilikuwa makao ya wasanii wengi waliochipukia katika tasnia ya injili. Wasanii Bahati alikuwa amewapa mkataba chini ya lebo hiyo ni miongoni mwao Weezdom, Peter Blessing, David Wonder miongoni mwa wengine.

Baada ya muda, Bahati walianza kuvurugana na wasanii hawa ndani ya EMB huku taarifa zikisema kwamba wasanii hao walikuwa na hulka ya kuenda kinyume na makubaliano ya kimkataba.

Migogoro hii ndani ya EMB ilifanya msanii Bahati kuifunga lebo hiyo na kuacha kuandikisha wasanii mikataba.

Kwa sasa, EMB inafanya muziki wa Bahati pekee baada ya kuifunga kutoka kuwaingiza wasanii wapya.