"Diamond alinifukuza Wasafi kisa kushiriki video ya Harmonize" - mcheza densi Sholey

Sholey ni mcheza densi maarufu ambaye ameonekana kweney video za wasanii wengi wa Bongo akianza na Maua Sama kabla ya kuingia Wasafi.

Muhtasari

• Mcheza densi huyo rasmi wa msanii Rayvanny alisema kipindi9 anafukuzwa hakuwa na mkataba wa kumzuia kutocheza na mtu yeyote nje ya Wasafi.

Mcheza densi wa Rayvanny, Sholey
Mcheza densi wa Rayvanny, Sholey
Image: Instagram

Mcheza densi rasmi wa msanii Rayvanny Sholey amefunguka kilichosababisha yeye kufukuzwa katika miradi ya video za msanii Diamond Platnumz.

Akizungumza na mwanablogu wa YouTube, Sholey ambaye amekuwa akionekana kwenye video za wasanii wengi tu ndani na nje ya WCB Wasafi tangu mwanzo kama vixen alisema alishtukia ghafla ametemwa kutoka kikosi cha vixens wa Diamond Platnumz.

Sholey alisema kwamba tangu mwanzo amekuwa akicheza kwenye video za ngoma za wasanii Diamond Platnumz, Harmonize, Rayvanny na hata Lavalava lakini hatua ya kutemwa kutoka kuonekana kwenye video za mhusika wa pale – Diamond Platnumz bila kujuzwa sababu ilihujumu nafsi yake sana mpaka kujihisi kukosa amani kuendelea kuwepo pale.

Alisema kwamba alihisi kutemwa kwake kulikuja pindi tu baada ya kuonekana kwenye wimbo wa Harmonize, Ushamba, wimbo ambao msanii huyo aliutoa muda mrefu tu baada ya kuondoka Wasafi kwa shari.

Ila alisisitiza kwamba yeye kucheza kweney wimbo wa Harmonize hakukuwa tatizo kwa sababu hakuwa na mkataba ndani ya Wasafi ulikuwa unamwekea mipaka ya wasanii wa kufanya kazi nao na wale wa kutofanya kazi nao.

“Kutoka tu popote nilijipata nimetolewa kwenye kazi za mhusika wa lile eneo. Mimi nilihisi ni kwa sababu ya kutokea kwenye wimbo wa Harmonize ‘Ushamba’ mimi ni mcheza densi tambua, nafanya kazi popote. Diamond hakuniambia kwamba Sholey naomba usicheze kwa mtu yeyote,” alisema vixen huyo.

Sholey alielezea kwamba wapambe wa Diamond ndio walimwambia atoke kwenye mradi wa wimbo wa Diamond ambao alikuwa ashiriki kucheza kwa kile walimtajia kwamba hana msimamo na ana tamaa ya kuonekana kote kote mpaka kwenye upande wa mahasidi wa Diamond – kwa maana ya kuonekana kwenye video ya Harmonize.