Huwa namtambulisha mwanangu kwa kila mpenzi wangu mpya - Amber Ray

Naingia kwenye uhusiano nikitarajia bora na yatafanikiwa. - Amber Ray.

Muhtasari

• Siingii kwenye uhusiano nikijiambia kwamba hii baada ya wiki mbili itaisha - Amber Ray.

Mwanasosholaiti Amber Ray amesema uhusiano wake na mwanawe upo wazi
Mwanasosholaiti Amber Ray amesema uhusiano wake na mwanawe upo wazi
Image: INSTAGRAM

Wiki hii kumekuwa na habari za chini yqa zulia kuhusu mwanamitindo Amber Ray kuwahi kupoteza ujauzito wa mfanyibiashara maarufu wa sekta ya matatu nchini Kenya, Jimal Rohosafi.

Ilisemekana kwamba Ray alifunguka alikuwa na ujauzito wa Jimal ila ukaharibika kwa bahati mbaya ambayo baadae alikuja kuitaja kuwa bahati nzuri kwani aliona Jimal alikuwa ameanza kujitoa kijanja.

Ray ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kiume sasa amefunguka jinsi anavyoishi na mwanawe huyo kwa jina Garvin.

Kupitia ukurasa wake wa YouTube akiendeleza kipindi chake cha ‘As It Is’ Ray alifunguka kwamba mwanawe huwa anawajua wanaume wote amabo anaingia kwenye mahusiano nao na wala haogopi kumtambulisha kwa wanaume hao ambao anaingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na kudumu nao kwa muda mfupi kabla ya kuwabadili kama nguo vile.

Amber Ray alisema kwamba yeye haogopi kumtambulisha kijana wake kwa wapenzi wake hao kwani dhumni lake ni kutaka Garvin ajue kwamba mamake si mtu mkamilifu na si kupenda kwake kuwa na mwanaume mmoja baada ya mwingine.

Alisema mwanawe sasa ni mtu mzima ambaye amejua mambo mengi tu na pindi anapomuuliza kitu huwa anamjibu jinsi ilivyo kwani akijaribu kuficha mwanawe tayari hugundua kuwa anamuongopea.

“Akianza kuniuliza siwezi kumsingizia kwani ninapomdanganya au kukwepa swali humkosesha raha na huwa ananipigia simu kila kukicha. Kwa hiyo natakiwa kumuelewa na sio kumuadhibu kihisia hivyo nimruhusu aingie kwa njia ambayo anajua kuwa huyu ni mpenzi wangu na anajua kuwa inaweza kufanya kazi au la,” alisema Amber Ray kwa ujasiri uliopitiliza.

Mwanasosholaiti huyo alielezea kwa masikitiko makubwa kwamba hata yeye si kupenda kwake kujikuta katika mahusiano mengi na wanaume tofauti kwani ni kitu ambacho kimekuja kujitokeza na si jambo ambalo analifurahikia kama ambavyo watu wanang’aka.

“Hii sio njia niliyojichagulia. Sikuwahi kutaka kuwa kwenye mahusiano mengi. Siingii kwenye uhusiano nikijiambia kwamba hii baada ya wiki mbili itaisha, naingia kwenye uhusiano nikitarajia bora na yatafanikiwa. Ninajaribu na nataka mwanangu anikumbuke kama mama huyo,” Amber Ray alisikitika.