"Nilifanya kazi Wasafi TV lakini sikuwahi lipwa hata shilingi" - Lukamba

“Mimi sijawahi kulipwa kazi yoyote ya Wasafi TV" - Lukamba.

Muhtasari

• Pia alisema kwamba Harmonize bado ni kipenzi cha msanii Diamond Platnumz ila kwa sababu ya biashara tu ndio ugomvi umeingia.

Msanii Lukamba akizungumzia madhira aliyopitia Wasafi
Msanii Lukamba akizungumzia madhira aliyopitia Wasafi
Image: Instagram

Aliyekuwa mpiga picha wa msanii Diamond Platnumz, Lukamba sasa amevua shati rasmi na kujitupa ulingoni kumenyana na bosi wake wa zamani kwa kile kinaonekana kama ni uadui mpya kabisa mwingine kati ya Diamond na mtu aliyekuwa chini ya lebo yake ya Wasafi.

Juzi Lukamba ambaye ameingia katika Sanaa ya muziki aliachia wimbo wenye utata mwingi ambao amewazungumzia wasanii wote waliokuwa ndani ya WCB na kuondoka – Rich Mavoko, Harmonize na Rayvanny.

Juzi alipokuwa akizungumza na wanablogu wa YouTube kuhusu utata unaozunguka wimbo huo, Lukamba alifunguka mengi ya kustaajabisha kuhusu bosi wake wa zamani Diamond Platnumz na lebo yake ya WCB Wasafi.

Lukamba alizungumzia suala la ugomvi kati ya Diamond na aliyekuwa msanii wake wa Kwanza katika lebo ya Wasafi, Harmonize.

Alisema kwamba Harmonize ndiye alikuwa kipenzi cha Diamond kwa muda mrefu na kwamba alitumia muda na gharama nyingi kumtoa Harmonize kuwa msanii mkubwa wengi wanayemfahamu sasa hivi.

Msanii huyo alisema kwamab ugomvi baina ya Harmonize na Diamond ulioteshwa na mashabiki ambao walianza kuwashindanisha, kitu ambacho Diamond hakupendezwa nacho.

“Mashabiki ndio chanzo na Harmonize kuwa na ugomvi na bosi wake. Ile milusi wakati wanamshindanisha Harmonize na Diamond, Diamond hakupendezwa nacho. Akawa anaona kwamba mashabiki wanampoteza kijana wake. Hakuwa anamaindi Harmonize, alikuwa anamaindi mashabiki wanaompoteza Harmonize,” Lukamba alifunguka.

Lukamba, akiwa kama mtu ambaye amekuwa nyuma ya Diamond kwa muda mrefu na kumjua kwa mapana na marefu alikanusha kabisa uwezekano wa kuwepo na uadui baina ya Diamond na Harmonize kabisa.

“Sijawahi kukaa hata siku moja nikaona anamuongelea kwa ubaya hivi na hivi, Hapana. Nafikiri mambo mengine yanakuwa labda ni kibiashara tu. Nafikiri hata Harmonize mwenyewe bado anaweza akawa na mapenzi makubwa sana na Simba lakini kwa sababu imetokea watu wameamua kuwashindanisha basi inabidi tu iwe hivo,” Lukamba alifunguka.

Msanii huyo aliwaingililia baadhi ya watangazaji katika stesheni ya Wasafi waliomponda vikali kwamba hana fadhila baada ya kutoka Wasafi na kuonekana kusema vibaya kuhusu kampuni zote zilizopo chini ya kivuli cha msanii Diamond Platnumz.

Alisema kwamba maana ya vyombo vya habari ni kuwa kati kati na kama ni mambo ya chuki basi waache chuki iwe baina yake na lebo wala si stesheni ya utangazaji ambayo inafaa kuwa kama refa.

Lukamba alifunguka kwamba alifanya kazi nyingi za kuhariri video za runinga ya Wasafi il ahata senti moja hakulipwa.

“Mimi sijawahi kulipwa kazi yoyote ya Wasafi TV. Mimi nilikuwa nafanya kwa mapenzi tu kwa sababu ya ndugu Diamond tu. Mimi niliajiriwa na lebo ya Wasafi lakini nilikuwa nafanya kazi mpaka za TV lakini sikuwahi pata hata shilingi kumi, Mungu shahidi,” alifoka.