Nashukuru Mungu nitatumbuiza Kasarani, Ruto aheshimiwe - Guardian Angel

Guardian Angel alifurahia kuteuliwa kama mmoja wa watumbuizaji katika hafla ya kuapishwa kwa Ruto Kasarani.

Muhtasari

• Bila kujali mtu huyo ni nani, lazima aheshimiwe nashukuru serikali inayokuja - Guardian

Msanii Guardina Anfel awataka Wakenya kumheshimu Ruto
Msanii Guardina Anfel awataka Wakenya kumheshimu Ruto
Image: Instagram

Mwanamuziki wa injili Guardian Angel amefurahia kugundua kwamba atakuwa mmoja wa watumbuizaji katika hafla ya kuapishwa kwa rais wa tano wa Kenya William Ruto.

Angel ambaye alikuwa ameandamana na mkewe Esther Musila alikuwa akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa Kasarani katika maandalizi ya shughuli hiyo ya Jumanne Septemba 13.

Angel alimsifiarais Ruto pakubwa na kusema kwamab ukombozi umefika Kenya kwani ishara yqa kiongozi wa taifa kuwatambua wainjilisti ni jambo zuri katika kuiweka nchi mikononi mwa Mungu.

Msanii huyo aliwataka Wakenya wote kumpa Ruto heshima anazostahiki kama rais ili kurahisisha uongozi wake na kikubwa kuzidi kumuweka katika maombi ili kupata busara itokayo kwa Mungu katika uongozi wake.

“Ni wakati ambapo urejesho umefika kwa injili. Kiongozi wa taifa anapomkiri Mungu sisi wananchi tutashindwaje kumkiri Mungu? Ni mahali pa sisi kurudi. Niliwaambia wakati wa mahojiano yaliyopita kwamba mnajiweka sawa na injili kwa sababu niliona yajayo ni injili na sasa wamejionea wenyewe,” Angel alisema.

“Kwangu mimi, sababu ya sisi kuwa hapa leo ni kusema kwamba uongozi wa taifa unapaswa kuheshimiwa. Hiyo ndiyo njia pekee ya kustawi. Bila kujali mtu huyo ni nani, lazima aheshimiwe nashukuru serikali inayokuja na namshukuru Mungu kwa kunipa nafasi hii ya kuwa sehemu ya sherehe za kuapishwa," Guardian Angel aliongeza.

Awali, mkewe Esther Musila pia alimsifia mama wa taifa ajaye Rachael Ruto kwa kusema kwamba mazoea yake ya kuomba ndiyo yalimwezesha Ruto kuibuka mshindi na hata kukiri kwamab ataanza kumuiga katika kuombea mumewe.

Itakumbukwa baada ya msanii Ringtone Apoko aliyekuwa anajiita mwenyekiti wa wasanii wa injili kung’atuka, Guardian Angel alijitangaza kuwa mrithi wake na kwa sasa ndiye mwenyekiti wa wainjilisti nchini Kenya.