Nikiwa mjamzito, Bahati lazima anisaidie kugeuka kitandani - Diana Marua

Diana alieleza kwamba kunenepa na kushindwa kutembea ndio baadhi ya mambo yaliyokuwa yanampa wasiwasi katika safari ya ujauzito.

Muhtasari

• Alidokeza kwamba hali haijakuwa mbaya katika ujauzito huu wa mwisho japo kuna changamoto kibao.

Diana Marua azungumzia wasiwasi wake huku akikaribia kujifungua
Diana Marua azungumzia wasiwasi wake huku akikaribia kujifungua
Image: Instagram

Mwanablogu na mwanamuziki Diana Bahati amefunguka sababu yake kuu kuwa na wasiwasi mkubwa katika safari yake ya ujauzito.

Akizungumza baada ya rafiki zake kumfanyia shtukizi la tafrija ya babyshower, Diana Bahati alitokwa na machozi ya furaha huku akiwashukuru rafiki zake kwa kuja kumfika karibu kwa msaada huku akitarajia kukaribisha uzao wat umbo lake kwa mara ya tatu kwa safari yake kama mama.

Aliwaambia wanablogu kwamba alikuwa na woga kuingia katika safari hiyo ya ujauzito kwa mara nyingine tena haswa baada ya kugundua kwamab alikuwa na ujauzito huo amabo awali alisema hawakuwa wametarajia kabisa pamoja na mpenzi wake mwanamuziki na mwanasiasa Kevin Bahati Kioko.

Marua alisema kwamba woga wake ulikuwa mkubwa kutokana na hali ambayo alikuwa amepitia katika ujauzito wake wa awali ambapo alisema huwa anaishiwa na nguvu na kuzimia wakati mwingine na hicho ndicho kitu alikuwa anakihofia kujirudia tena katika ujauzito wa tatu.

Lakini alidokeza kwamab ujauzito huu umekuwa tofauti kidogo kwake kwa heri hata kama safari yenyewe imekuwa yenye changamoto si haba.

Mwanamuziki huyo wa kutema mistari alisema kila mara anapokuwa na ujauzito, huwa anishiwa na nguvu hata kushindwa kugeuka. Alisema mumewe Bahati ndiye humsaidia kugeuka kitandani.

“Ninahangaika na mimba katika suala la kuzimia, kunenepa...ninapokuwa karibu na tarehe yangu ya kujifungua (miezi saba hadi nane), siwezi kutembea. Hata nikiwa kitandani, Bahati lazima anisaidie kugeuka ili kupata hali kama hiyo, ndilo lililokuwa linanivunja moyo kwa sababu sikuwa tayari kupitia chanamoto hizo mara nyingine tena,” alisimulia.

Marua awali baada ya kuutambulisha ujauzito wao, katika msururu wa video alionekana kumrai mumewe kwamab akubali huo uwe ndio ujauzito wake wa mwisho kwani huwa anapitia chanamoto nyingi japo hakuzitaja.

Alimtaka Bahati kukubali kufanya vasektomia ili kuepusha mimba zisizopangiwa kama hiyo amabyo alidokeza ilikuja pasi na kupangiwa.

“Kujua kuwa ninakaribia kuona uso wako mdogo mzuri, cheza na vidole vyako vidogo, kukushika kwenye chuchu zangu kila siku ninapokutazama ukikua na kukuvutia wakati wote, sio kweli kabisa,” marua aliandika kwenye moja ya video zake Instagram.