Nishawahi kukamata 2Bn kwa mkupuo, msinichukulie poa - Barnaba Classic

Sitegemei muziki tu, nina mirija mingi ya kuniingizia hela - Barnaba,

Muhtasari

• Nimekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu, mitikasi yangu ni mingi, sitegemei tu muziki - Barnaba.

msanii Barnaba Classic awasuta wanaosema hawezi kumiliki bilioni mbili kwa mkupuo.
msanii Barnaba Classic awasuta wanaosema hawezi kumiliki bilioni mbili kwa mkupuo.
Image: Instagram

Msanii Barnaba Classic baada ya kuachia albamu yake mpya, amekuwa akizunguka katika sehemu mbali mbali ndani na nje ya Tanzania ili kuifahamisha albamu hiyo kwa wana katika kitaa.

Juzi kati katika ukurasa wake alizungumza kwamba amewahi kukamata kiasi cha bilioni mbili pesa za Tanzania kwa mkupuo na kuwataka watu wasimchukulie poa.

Kweney upande wa maoni, wengi walionekana kumkataa kwa kusema kwamba hakuwa na hajawahi kuwa na uwezo wa kumiliki kiasi kikubwa cha pesa kama hicho kwa wakati mmoja.

Sasa Barnaba katika kipindi cha Refresh cha Wasafi, alifunguka wazi kwa kusema kwamba ukweli wake ndio huo na hana faida yoyote katika kula uongo.

Alisema aliwahi pokea kiasi cha bilioni 2 kwa mara moja na pia kusisitiza kwamba alinukuliwa vibaya kwani kwa sasa hivi kuna uwezekano anapokea kiasi zaidi ya hicho.

“Watu wameninukuu vibaya, pesa ipi nimewahi kuishika kwa mkupuo, nikasema ni bilioni mbili. Ni kweli nimeshawahi kukamata bilioni mbili kwa mara moja lakini sasa hivi kuna uwezekano ninapata nyingi zaidi ya hizo,” Barnaba alilainisha mambo.

Barnaba alisema hajui ni kwa nini watu wanakaa kama vile hawamuamini katika maneno hayo na kuongeza kwamba pengine ni kutokana na hali yake ya kutoweka wazi kila kitu kwenye mitandao aghalabu.

“Mimi si mzungumzaji sana kwenye mitandao na lile lilikuwa ni swali niliulizwa na mtangazaji ni kasema ni bilioni mbili pap, lakini yaezekana sasa hivi ninazidi hapo. Nimekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu, mitikasi yangu ni mingi, sitegemei tu muziki, nina mirija mingi ya kupata hela. Kwangu bilioni mbili si kitu, mafanikio hayasemwi,” Barnaba Classic aliwasuta wale wanaomsuta kwamba hana uwezo wa kushika kiasi hicho.