Paula amkubali Harmonize, amsifia na kumuita 'Baba', hii ina maana gani kwa Rayvanny?

Ama kweli siku zote aliyemuoa mama ndiye baba!

Muhtasari

• Kumkubali kwake Harmonize kunatia msumari wa mwisho katika jeneza la msanii Rayvanny.

Bintiye Kajala Masanja na babake wa kambo, Harmonize
Bintiye Kajala Masanja na babake wa kambo, Harmonize
Image: Instagram

Utata unazingira mahusiano ya Harmonize, mchumba wake Kajala Masanja na binti yake Paula Kajala umechukua mkondo mwingine baada ya binti huyo wa Kajala kumtaja Harmonize kama babake.

Kwa faida ya kumbukizi tu ni kwamab Kajala Masanja alikuwa ni mke wa mzalishaji maarufu wa ngoma za bongo tangu zamani P Funk Majani ambayo enzi wakiwa wanandoa walifanikiwa na mtoto Paula.

Baadae walitengana kutokana na sababu za kibinafsi na kila mmoja Kwenda zake ambapo, mama aliondoka na mtoto na miaka kadhaa baadae akajipata katika mahusiano na msanii Harmonize, japo mahusiano yao pia yamekuwa yakisimangwa kutokana na upana uliopo kati ya umri wao, Kajala akiwa amemzidi Harmonize kwa miaka kumi na ushee.

Harmonize na Kajala mahaba yao yalifika kipindi fulani yakakwamishwa baada ya kugundulika kwamab Harmonize alipewa kubonyeza yeye akataka kubonyeza kabisa kumiliki kuku na kifaranga wake – kwa maana kwamba alianza pia kumtolea macho ya kumtamani binti Paula Kajala.

Kipindi hicho Kajala yupo kwenye mahusiano ya mwanamuziki Rayvanny, na sakala zima lilichukua mkondo tofauti kabisa mpaka Kajala kumtoroka Harmonize kwa ajili ya usalama wa bintiye.

Hivi karibuni Harmonize walirudiana na Kajala na kwa upande mwingine Paula wakatengana na Rayvanny. Paula baada ya Harmonize kumvisha mamake pete ya uchumba, alielekea kweney Instagram yake na kupakia picha ya zamani akiwa na mamake na babake halisi mzee P Funk Majani na kusema hiyo ndio familia yake halisi anayoitambua, huku akionekana kumkana kabisa Harmonize licha ya kumchumbia mamake.

Ila hakuna mkate mgumu mbele ya chai na wenye midomo wanasema aliyemuoa mama ndiye baba.

Kajala sasa amemkubali Harmonize kama babake, na ameonekana kuufurahia uhusiano wake na mamake hadi katika biashara ambayo Kajala ndiye meneja wa kazi za muziki za Harmonize.

Jumapili Paula alipakia video ya mamake na babake wa kambo, Harmonize wakicheza wimbo wao mpya ‘Amelowa’ kwenye Instagram na kuandika maneno ya kumsifia Harmonize kwa kumuita baba.

“Nyinyi, wote hamko tayari kwa dude hili jipya. Baba unajua mpaka unajua tena, Harmonize,” Paula aliandika kwenye instastory yake, kuonesha kwamba amemkubali Harmonize kama baba.