Khadija Kopa ajibu jamaa aliyemdhalilisha na mwanawe, amtaka Zuchu kutoenda polisi

Ostaz Juma alimdahlilisha Kopa na Zuchu kutokana na maumbile yao ya kimwili.

Muhtasari

• Khadija Kopa alisema hana muda wa kujibizana na jamaa huyo na kumkanya Zuchu dhidi ya kumchukulia hatua za kisheria.

• Awali Zuchu alikuwa amekerwa na Ostaz na kuahidi kupambana naye kisheria.

Khadija Kopa na binti yake Zuchu
Image: HISANI

Juzi kumekuweko na Sakata la msanii Zuchu kuchukizwa na hatua ya mwanaume mmoja kwa jina Ostaz Juma kufanay video aliwadhalilisha yeye na mamake kutokana na maumbile ya miili yao.

Katika video hiyo na ambayo tulikusimulia kisa hicho awali, Ostaz Juma alifanya klipu akisema kwamba Zuchu huku mbeleni atakuja kuchukua maumbile kama ya mamake kwa maana ya kuwa na maziwa kubwa pamoja na mwili wa kibonge, tofauti na sasa hivi alivyo mwembamba kiasi.

Kwa upande mwingine pia mwanaume huyo alisema kwamab Zuchu hajabarikiwa upande wa taili za nyuma na kumuusia Diamond kama anampenda basi amkubali kweli jinsi alivyo huku akiwa na matumaini kwamab mbeleni atakuja kurithi kila kitu kwa mamake kutoka sauti ya kuimba hadi umbile.

Jambo hili lilimgadhabisha sana Zuchu ambaye kupitia ukurasa wake wa Instagram aliachia ujumbe mrefu akiapa kumchukulia hatua jamaa huyo kwa kumdhalilisha kimaumbile yeye pamoja na mamake Khadija Kopa.

Khadija Kopa ambaye ni mwanamuziki mkongwe na mipasho na rusha roho za Taarab alifikiwa na Sakata hili ambapo kupitia mahojiano ya simu alisema yeye hana muda kabisa wa kujibizana na jamaa huyo aliyemdhalilisha.

Kopa alisema kwamba yeye atalipishiwa na Mungu na hata kuonekaan kutofurahia hatua Zuchu anazotaka kuzichukua dhidi ya jamaa huyo. Alimkanya mwanawe kuacha kumpeleka Ostaz polisi na kusema kwamba kila kitu wamuachie Mungu.

“Nakwambia mimi sasa hivi sina muda wa kuzungumzia jamaa huyo, sina muda huo. Mimi naridhika na maumbile yangu Mungu ashaniumba vile vile, namshukuru Mungu,” Mamake Zuchu alisema.

Wengi walidhania mwanaume huyo baada ya kutishiwa polisi atanywea na kuomba samahani lakini aliendelea mbele kutoa video nyingine akisema kwamba Zuchu hawezi kumtishia eti anadhalilisha mzazi wake kwani yeye katika baadhi ya nyimbo ameimba akiwataja wazazi wa watu kwa njia Ostaz alisema ni ya kuwadhalilisha pia, kwa hiyo alichokifanya ni ngoma droo.