Kuwa single kunanipa muda wa kusoma Biblia, weeh Jeremiah aliteseka!! Aliumia - Njambi

Njambi alijipatia umaarufu katika igizo la The Real Houswehelps of Kawangware.

Muhtasari

• Katika mahojiano na Eve Mungai, Njambi alisema aliachia ndoa yake kutokana na kudundwa vibaya na mpenzi wake.

Mwigizaji Njambi
Mwigizaji Njambi
Image: Instagram

Aliyekuwa mwigizaji wa The Real Househelps of Kawangware, Njeri Gachomba almaarufu Njeri hivi karibuni alidokeza kuvunjika kwa ndoa yake kwa kile alisema ni manyanyaso yasiyo na mwisho.

Njeri katika mahojiano na mwanablogu wa YouTube Eve Mungai alisema kwamab mzazi mwenzake alikuwa ni mtu wa vijisababu na figisu figisu  kumtesa kila mara na ndio ilikuwa sababu kubwa ya kutia guu nje ya ndoa yake.

Alifunguka kisa kimoja aliporudi nyumbani simu ikiwa imezima na mumewe alimcharukia kwamba alikuwa anachepuka ndio maana simu yake ilikuwa imezima.

Siku moja nilienda kutembea na marafiki zangu na niliporudi simu yangu ilikuwa imezima.Niliporudi alidai na kuanza kutafuta ushahidi kwa sababu alidhani nilikuwa na mwanaume. Aliposhindwa kupata ushahidi alinipiga jicho na simu. Nilikuwa na jicho jeusi kwa mwezi mmoja,” Njambi alisema.

“Aibu ya kuwa katika uhusiano au kuwa mwathirika wa uhusiano wa matusi kwa kweli iliniweka ndani kwa muda mrefu zaidi kuliko nilivyopaswa kuwa. Hatimaye nilipata ujasiri na ninashikilia hilo” Njambi alidhibitisha kupata suluhu la mateso yake kwenye ndoa.

Sasa mwigizaji huyo baada ya takribani mwezi mmoja kukaa peke yake, amefichua jinsi maisha ya kuwa bila mpenzi yamekuwa katika kipindi hicho kifupi tangu kung’atuka kwenye ndoa yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Njambi ameandika kwamba mtu ukiwa singo bila mtu huwa unapata muda mwingi sana wa kutathmini maisha yako na kufanya mambo ya maana kama kusoma Biblia.

Kwa kile kilionekana kama amekuwa akijishughulisha sana na kusoma Biblia kitabu cha Jeremiah, Njambi alisema kwa utani kwamba kweli nabii huyo wa Mungu katika Biblia aliteseka kweli.

“Kuwa single kunanipa muda wa kusoma Biblia, weeh... Jeremiah aliteseka!! Aliumia,” Njambi aliandika na kufuatisha maneno hayo na emoji za kucheka.