Nadia na Arrow Bwoy kuachia wimbo kwa ajili ya mwanao Kai

Mukami na Arrow Bwoy walitangaza kupata mwanao huyo miezi kadhaa iliyopita

Muhtasari

• Kupitia Instagram yake, Nadia Mukami amedokeza kwamba wimbo huo tayari umepikwa ukaiva na kesho majira ya asubuhi watauachia kwenye YouTube yake.

Nadia Mukami na Arrow Bwoy kuachia wimbo kwa ajili ya mwanao
Nadia Mukami na Arrow Bwoy kuachia wimbo kwa ajili ya mwanao
Image: Instagram

Mwanamuziki Nadia Mukami na mumewe Arrow Bwoy wametanagza kwamba waliingia studioni na kurekodi wimbo wa kumsifia kifungua mimba wao Kai.

Kupitia Instagram yake, Nadia Mukami amedokeza kwamba wimbo huo tayari umepikwa ukaiva na kesho majira ya asubuhi watauachia kwenye YouTube yake.

Akiandika maoni kwenye picha yao ya pamoja iliyopakiwa na Nadia ikimuonesha amesimama na mtoto Kai mkononi huku mumewe Arrow Bwoy ameketi, Msanii huyo alidokeza kwamba ngoma hiyo itaenda kwa jina Kai Wangu.

Mukami na Arrow Bwoy walitangaza kupata mwanao huyo miezi kadhaa iliyopita baada ya kufungua wakfu wao wa Lola na Safari unaoshughulikia masuala ya kina mama wajawazito.

Awali Nadia na Arrow Bwoy walitangaza kwamba jina hilo la wakfu wao lilitokana na majina mawili ambayo walikuwa wameteua kwa ajili ya mwanao wa kwanza ambaye kwa bahati mbaya ujauzito wake uliharibika.

Suala la Nadia kuwa mjamzito waliliweka chini ya zulia kwa muda mrefu na aliyekuwa mtangazji na mchekeshaji Jalang’oo alifichua ujauzito huo na kuzua mzozo mkali baina yake na familia hiyo iliyomtuhumu kwa kuingilia mambo yao, hapo ndipo walifunguka changamoto walikuwa wanapitia kuwafanya kutofichua habari za ujauzito kwa sababu walikuwa wamepoteza ujauzito wa kwanza na walikuwa katika safari ya kupona ambapo Jalang’o aliwatanusha.

Jalang’o aliwafuata na kuwaomba radhi kwa kuweka wazi habari hizo katika kile alijitetea kwamba hakuwa anajua kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia.