Mwakani nitamiliki private jet, nisipofanikiwa mniite mbwa - Madee

Msanii huyo aliwahimiza watu kuropoka maneno kwani yanaumba

Muhtasari

• “Msiogope kuropoka vijana.. maneno yanaumba" - Madee.

Madee asema mwishoni wa mwaka atamiliki ndege ya kibinafsi
Madee asema mwishoni wa mwaka atamiliki ndege ya kibinafsi
Image: Instagram

Msanii made Ali kutoka Tanzania ametangaza kwamba mwaka kesho atamiliki ndege ya kibinafsi, Private Jet.

Kupitia Instagram yake, Madee alikuwa anamtakia heri njema ya siku ya kuzaliwa msanii mwenzake Dogo Janja. Alipakia video ya zamani kabisa Dogo Janja alikwa mtoto mdogo akihojiwa ambapo anasikika akisema akija kuwa mkubwa angependa kuwa msanii mkubwa na kupanda ndege.

Dogo Janja amabye kwa sasa ni mtu mzima alishalitengeneza jina lake na kuwa kubwa kwenye muziki wa rap ya Kiswahili na kama ndege ameziabiri sana.

Madee alitumia video hiyo kuwapa watu himizo kwamba wasiogope kuropokwa kwani maneno huumba. Alitolea mfano Dogo Janja kwenye video hiyo enzi akiwa mdogo alifanya udhubutu wa kuropokwa na kweli yale yote aliyoropokwa yalikuja kutimia.

“Msiogope kuropoka vijana.. maneno yanaumba... kijana mwenzenu huyu hapa,😂karopoka na maneno yameumba... alitamani kua mwanamziki mkubwa.. I think amekua, alitamani kupanda ndege.. kapanda wee mpaka anaamua kujirusha angani.. na Leo ndio siku AMEZALIWA.. happy birthday son,” Madee aliandika.

Alisema naye ameropokwa kwamba ifikapo mwisho wa mwaka huu basi ataufunga mwaka akiwa na ndege yake ya kibinafsi. Alikula Yamini kwamba iwapo hatomiliki ndege ya kibinafsi basi watu wote wana haki kabisa ya kumwita mbwa tena wa kiume.

“Oya wana TUROPOKE TUSIOGOPE!! Mfano mimi mwakani ntamiliki private jet... nisipofanikiwa mniite Dog lakini dume.. nipo pale nimekaa,” Madee aliwahakikishia mashabiki wake.

Kwenye post hiyo, msanii Dogo Janja alimshukuru Madee kwa kumpa ujasiri wa kutusua kwenye gemu la rap ya Kiswahili japo kulikuwa na mawimbi makali.

Baba Confidence uliyonijengea inanifanya nikae mezani na mtu yoyote na tukaongea lugha moja! 🙏🏼 zamani nlikua naskiaga tu usiwarithishe watoto mali, wafunze kuzitafuta! Na nimeiona kwako! Shukran sana! Na ndani ya Miaka 5 tukijaaliwa Uhai,Ntakua Na Brand Ya Simu Kalii Sanaa kushinda hizi na itakua inamilikiwa Na JANJAROOO!” Dogo Janja alimshukuru.