Siwezi kuwarudisha kazi Eli Khumundu na Litiema, nitawatafutia kwingine - Jalang'o

Wawili hao walikuwa wafanyikazi wa Jalang'o kabla ya kumuibia milioni moja kutoka kwa gari na kutoroka nazo

Muhtasari

• "Ila nitawatafutia kazi kwingine wafanye,” Jalang’o alisema ukweli wake.

Jalang'o asema hawezi kuwarudisha kazi Eli Khumundu na Litiema

Mbunge wa Lang’ata Phelix Odiwuor almaarufu Jalang’o amefunguka baada ya aliyekuwa mfanyikazi wake El Khumundu kusema kwamba anajuta kumuibia na anataka amrudishe kazi kwani ndoa yake iko mashakani.

El Khumundu na mwenzake Morrison Litiema walikuwa ni wafanyikazi wa Jalang’o nyumbani kwake jijini Nairobi na miezi michache iliyopita walimuibia kima kilichotajwa kuwa shilingi million moja na kutoroka nazo.

Jalang’o aliwarai kurudisha pesa hizo na kuwaahidi hangewachukulia hatua, ahadi ambayo kweli aliitumia baada ya vijakazi hao kurudisha kiasi cha pesa walizokuwa wamebakisha.

Ila Jaang’o hakuweza tena kuwarudisha kama vijakazi wake. Aliwafuta na miezi kadhaa baadae wawili hao walianza kulia wakisema wanajutia kitendo cha kumuibia bosi wao.

Khumundu alimtaka Jalang’o kuwasamehe na kuwarudisha kazi kwa kile alisema familia yake iko katika hali mbaya ya njaa na ikiwa hali itaendelea basi huenda familia ikasambaratika na mkewe kumtoroka.

Jana katika mahojiano na mwanablogu wa YouTube, mbunge Jalang’o alizungumzia suala hilo ambapo alisema kamwe hawezi kuwarudisha kazi waliokuwa vijakazi wake hao.

Alisema kwamba kama ni kuwakwamua njia pekee ni kuwatafutia kazi kwingine ya kufanya lakini si kuwarudisha katika boma lake abadan asilani.

“Kwanza labda nitawatafutia kazi kwingine kwa sababu ukweli wamejuta walichokifanya kwangu. Wamesema ni shetani aliwaingilia ila ukweli ni kwamba kama ningetaka kuwasaidia, kuwarudisha kwangu itakuwa vigumu mno kwa sababu jamii nzima kule ninaishihaitonikubalia kuwarudisha. Wameshawajua kama watu wabaya. Ila nitawatafutia kazi kwingine wafanye,” Jalang’o alisema ukweli wake.

Mbunge Jalang'o asema hawezi kuwarudisha kazi waliokuwa vijakazi wake

Image: Facebook