Jovial awataka watu wakome kumpa shinikizo la kurudisha mkono kwa jamii

Kurudisha mkono ni suala binafsi kati yangu na Mungu - Jovial

Muhtasari

• Alisema amekuwa akipokea shinikizo katika DM watu wakimtaka kurudisha mkono kwa kuwasaini wasanii chipukizi.

• "Na tafahdali acha iwekwe wazi kwamba kusaini msanii si kurudisha mkono kwa jamii bali ni biashara." - Jovial.

Jovial awataka watu wakome kumpa shinikizo la kusaii wasanii wapya
Jovial awataka watu wakome kumpa shinikizo la kusaii wasanii wapya
Image: instagram

Mwanamuziki wa kizazi kipya nchini Kenya Jovial amefunguka jinsi watu wanamweka chini ya shinikizo katika DMs zake wakitaka washike mkono wasanii chipukizi.

Suala hili linaloonekana kuwa chukizo kubwa kwake linamfanay kuhisi kwamba watu haswaa mashabiki wake wanamkemea kwa kuwa na mafanikio mwngi zaidi ila bado hajamshika na kumuinua msanii mwingine, au hata kumsaidia kupata mkataba katika rekodi lebo.

Akizungumzia suala hili kwenye Instastories zake, Jovial kwa gadhabu alisema suala hilo linamfanya aonekane mtu mweney roho mbaya na kuwataka watu kukoma kumshinikiza. Aisema kuna njia tofauti amabzo msanii anaweza tumia ili kufanay malipizi kwa jamii na si tu kwa kumshika msanii mkono.

Kulingana na Jovial, kurudisha mkono katika jamii ni siri kati ya mtu na Mungu wake na si lazima aanike kila kitu amabacho anafanyia jamii kwenye mitandao ya kijamii.

“Kuna huu usaliti wa kihisia ambao ninaupata kwenye DMs zangu kuhusu kurudisha mkono katika jamii, haswaa kuwasaini wasanii wapya. Sawa, kurudisha mkono katika jamii ni suala la binafsi kati ya mtu na Mungu. Huwa sifanyi kuanika katika gwaride la mitandao na kijamii,” Jovial alisema.

Mkali huyo wa kibo cha Jeraha alizidi kubainisha kwamba watu wanafaa kujua kusaini msanii kwenye lebo si njia moja ya kurudisha mkono katika jamii bali hiyo ni biashara kwa sababu mtu unawekeza katika kipaji chake.

Alisema yeye ameona jinsi lebo nyingi zinasumbuana na wasanii kwa kuwapa mkataba wakienda kinyume nao wanamalizia mahakamani na kusema hiyo ndio sababu ilifanya asichukue mkondo huo.

“Na tafahdali acha iwekwe wazi kwamba kusaini msanii si kurudisha mkono kwa jamii bali ni biashara. Nakupa mkataba, unafanya kazi tunarudisha pesa, ukifeli ninavunja mkataba wako na tunaishia mahakamani. Nilichagua kutochukua njia hiyo kwa hiyo achana kabisa na kunichukiza kihisia. Baraka zangu zinafunguka kila siku,” Jovial alimaliza.