Kweli hamchoki? Endeleni tu - Lilian Ng'ang'a awajibu wale wanaolinganisha Juliani na Mutua

Watu mitandaoni walikuwa wanafananisha picha ya Mutua akiwa Markani na begi na ile ya Juliani akiwa amesimama na kiti cha mtoto

Muhtasari

• Ng'ang'a na Mutua waliachana Octoba mwaka jana baada ya kukaa pamoja kwa miaka 10 na mwezi mmoja baadae aliingia katika mahusiano na msanii Juliani.

Image: Instagram

Jana baada ya picha ya aliyekuwa gavana wa Machakos Alfred Mutua kuonekana akiwa New York Marekani akiwa ameshikilia begi lake na kuvaa tabasamu la karne.

Wakenya wadadisi wa mitandao waliibuka na kile kilichoonekana kama meem ambapo walitoa picha ya Juliani, msanii wa kutema mistari akiwa pia ameshikilia kiti cha mtoto wake kinachosukumwa kama begi na kuanza kulinganisha picha hizo mbili.

Kilichowafanya watu kufanya ulinganisho huu ni kutokana na Sakata lililopo baina ya hao wawili ambao mwanamama Lilian Ng’ang’a alikuwa mke wa Mutua kabla ya kumuacha na kuoana na msanii huyo.

Hivi karibuni Mutua ambaye ni mmoja wa viongozi wa mrengo wa serikali ya Ruto alidokeza kwamba baada ya mahusiano yake na Ng’ang’a yaliyodumu kwa miaka 10 kusambaratika, ana furaha na hafikirii kuoa tena.

Gumzo la picha za Juliani na Mutua wakilinganishwa liiendelea leo baada ya mwanablogu Andrew Kibe kufanay mitikasi yake na kumsifia Mutua kwa kuirejesha furaha yake kwa kuivunja ndoa yake na Ng’ang’a.

Kibe alizidi kumzomea mwanamke huyo ambaye sasa ni mama wa mtoto mmoja waliyezaa na Juliani kwa kusema kwamba Mutua sasa ako vizuri na yeye amerejea nyumbani kufanay malezi ya mtoto.

“Pengine jambo zuri zaidi kutokea kwa mohine huyu ni yule kastro kumuacha. Anatamba kiserikali sasa huku mwingine akirudi nyumbani kulea watoto. Gaddamn,” Kibe alisema.

Image: Instagram

Hili lilionekana kuzidisha gumzo hilo la kulinganisha picha za wanaume wawili wa Lilian Ng’ang’a ambaye alielekea kwenye Instastory yake na kuwapasha vikali wale wanaoendeleza gumzo hilo.

“Nimeona hadithi isiyo na kina ambayo kila mtu anajaribu kunivuta. Kweli hamchoki...Endeleni tu. Acha niendelee na siku yangu na mtoto wangu mdogo,” Lilian Ng’ang’a alijibu.