"Nataka wazee, vijana hapana" Mwinjiliti Ruth Matete adokeza miaka 2 tangu kifo cha mumewe

Ruth Matete anarejea katika tasnia ya mapenzi miaka 2 baada ya kifo cha mumewe

Muhtasari

• Kwa hivyo nahitaji mtu anayeelewa - Matete aliweka wazi.

Mwimbaji Ruth Matete asema anataka mpenzi
Mwimbaji Ruth Matete asema anataka mpenzi
Image: Instagram

Mwinjilisti Ruth Matete amerudi tena sokoni baada ya muda tangu kifo chenye utata cha mumewe Mnigeria, Sakata ambalo lilimzunguka na mpaka kumhusisha kuwa na mkono katika kifo cha rais huyo wa Kigeni.

Matete sasa anasema kwamba yupo tayari kabisa kuogelea kwenye kidimbwi cha mahaba ila kwa sharti!

Matete alitoa sharti kali kwamba hata kama ako singo na anataka kutafutwa, nafasi hiyo si kwa kila mtu bali ni kwa watu wazima waliokomaa kabisa. Aliwataka vijana wadogo kukaa mbali kabisa na wasijaribu kumtafuta.

“Nataka wazee vijana hapana. Mimi sio mtoto bwana. Nitafikisha umri wa miaka 37 mwaka ujao. Kwa hivyo nahitaji mtu anayeelewa unajua umefanya nini...piga risasi yako ukitaka kupiga,” Matete alitoa sharti.

Wakati wa mahojiano na Lupaso, Ruth Matete alibainisha kuwa alikuwa hajaolewa na yuko tayari kujaribu bahati na jinsia tofauti. Alisema kwamba hakuwa akitafuta mtu na alirejezea Biblia, akisema kwamba wanawake walipaswa kufukuzwa, si vinginevyo.

“Niko single sana. Kuna single na kuna single sana. Niko single sana. Nataka kutafutwa. Biblia inasema mwanamume...si mwanamke. Hiyo nayo hatuwezi kubadilisha dhana hiyo kwamba mwanamume ndiye anafaa kumtafuta mwanamke, nangoja kutafutwa,” Matete alisema.

Ruthu alikuwa ameathirika sana kisaikolojia kutokana na matukio yaliyofuatia baada ya kifo cha mumewe. Alijipa miaka miwili ili kutuliza akili na sasa anahisi yuko sawa kujaribu karata katika uwanja wa mapenzi.

Mapema mwaka huu, mama wa mtoto mmoja alisherehekea mwenyewe kwa kuwa mwanamke mwenye nguvu na kujiinua baada ya kifo cha mumewe. Mwimbaji huyo alibaini kuwa alikuwa na ujauzito wa miezi minne wakati mume wake alipomwacha kwenda mbinguni na alihuzunika.