Acha uchonganishi, mimi namjua Diamond vizuri kukuliko - Lukamba amsuta H-Baba

Hakuna sehemu niliwahi sema simba hajanisaidia - Lukamba.

Muhtasari

• Acheni hizo mwacheni mtu afanye maisha yake acheni uchonganishi,” Lukamba alimfokea H-Baba.

Lukamba amchana H Baba kwa kusema alitoka Wasafi kwa shari
Lukamba amchana H Baba kwa kusema alitoka Wasafi kwa shari
Image: instagram

H-Baba ndiye chawa wa hivi karibuni kujiunga katika pango la simba Diamond Platnumz baada ya kuramba dili la kuwa balozi wa Wasafi bet yake Mond.

Katika siku za hivi karibuni, msanii huyo mkongwe ameonekana katika mahojiano na wanablogu wengi tu akiwasuta wale wote wanaooonekana kutokula kutoka sahani moja na Diamond Platnumz.

Juzi ameonekana kwenye mahojiano ambayo kando na awali alikuwa anamwingilia Harmonize, safari hii alimchana makali aliyekuwa mpiga picha wa Diamond, Lukamba.

Lukamba aliondoka Wasafi miezi miwili iliyopita na baada ya kufungua afisi zake kama msanii huru, alionekana kutomkubali aliyekuwa bosi wake na hata kuonekana kumchana kwa kumfagilia mbaya wake, Harmonize.

H-Baba amejivika viatu vya uchawa ambapo amechukua ugomvi kati yake na Lukamba na kumzomea kwamba hafai kumdharau Diamond kwani yeye ndiye aloyemfanya kuwa maarufu, kupata riziki, mke na hata hela za kufungua biashara yake mwenyewe.

Maneno haya hayakuenda vizuri na Lukamba ambaye alipakia mahojiano hayo ya H-Baba na kumzomea vikali kwamba ni njaa tu inamsumbua na ni lazima abweke ili kupata kitu.

Pia alizidi kumkunjia kwamba yeye ndiye anamjua na kumfahamu vizuri Diamond na wala si H-Baba ambaye ameingia pale juzi.

“Kaka mimi namjua simba kuliko wewe namkubali simba kuliko wewe na hata yeye pia anajua hilo …hakuna sehemu niliwahi sema simba hajanisaidia halafu hii kauli kwamba ‘alitoka vibaya’ wewe unajua mikataba yetu mmekazania katoka vibaya vibaya kuna sehemu nishawahi mvunjia heshimaa? Acheni hizo mwacheni mtu afanye maisha yake acheni uchonganishi,” Lukamba alimfokea H-Baba.