Mark Zuckerberg na mkewe watangaza kutarajia mtoto wa tatu

Baba huyo wa watoto wawili wa kike aliweka wazi kwamba mkewe ni mjamzito tena kwa mtoto wa tatu binti.

Muhtasari

• “Upendo mwingi. Ninafurahi kuwataarifu kuwa Max na August wanapata dada mpya mwaka ujao!” Mark Zuckerberg

Mark Zuckerbeg na Priscilla Chan watangaza mimba ya tatu
Mark Zuckerbeg na Priscilla Chan watangaza mimba ya tatu
Image: Facebook

Mmiliki wa kampuni kubwa kabisa ya mitandao ya kijamii, Meta Mark Zuckerberg ametangaza kwamba mwaka ujao yeye na mkewe wanatarajia mtoto wa tatu.

Mkwasi huyo wa Facebook aliweka wazi kupitia mtandao huo kwamba ifikapo mwaka wa 2023, atapata mtoto wa tatu ambaye alidokeza kuwa atakuwa wa kike.

“Upendo mwingi. Ninafurahi kuwataarifu kuwa Max na August wanapata dada mpya mwaka ujao!” Mark Zuckerberg aliandika.

Zuckerberg alifunga pingu za maisha na mke wake Priscilla Chan mwezi Mei mwaka 2012 na katika safari yao ya miaka kumi kwenye ndoa, wawili hao wana watoto wawili wa kike ambao ni Max Chan na August Chan.

Ni sahihi kusema kwamba Tajiri huyo atakuwa baba wa binti watatu majaaliwa mwaka kesho na mashabiki wake wengi wamefurika Facebook kumhongera baada ya kutangaza habari hizo.

“Hiyo inashangaza! Hongera! Kwa bahati Max atakuwa na umri wa kutosha kumlea mtoto hivi karibuni” mmoja kwa Vivian Wu aliandika.

“Ndiyo!!!! Nimefurahishwa na wewe na Prisila kuleta msichana mwingine mwenye nguvu na siku moja kuwa mwanamke ulimwenguni,” Mwingine alisema.

“Ninapenda tu August kwa sababu mimi na watu wengine wengi muhimu kote ulimwenguni tulizaliwa mnamo Agosti! Kwa umakini zaidi, hongera! Baraka kwako na kwa vizazi vyote ambavyo vitabadilisha ulimwengu huu kupitia wewe!” Joys Kimani aliandika.