TikToker Kinuthia ahusika katika ajali ya barabarani akimpelekea mamake zawadi

Kinuthia alikuwa akielekea kwa mamake kumshtukizia kwa zawadi ya mapema ya siku ya kuzaliwa.

Muhtasari

• Nilikuwa nataka kumshtukizia mama yangu kwa zawadi ya mapema ya kumtakia heri njema ya siku yake ya kuzaliwa lakini nikapata ajali - Kinuthia.

Kinuthia ahusika katika ajali ya barabarani
Kinuthia ahusika katika ajali ya barabarani
Image: Instagram

Mwanatiktoker Kelvin Kinuthia asubuhi ya Alhamis alihusika katika ajali ndogo ya barabara akiwa njiani kuenda kumshtukizia mamake nyumbani.

Kinuthia alipakia video ya magari hayo mawili moja likiwa la kwake ambayo yalikwaruzana mbele kidogo na kusema kwamab siku yake imepata mwanzo mbaya sana.

Alidokeza kwamba hivi karibuni mama yake atasherehekea heri njema ya siku yake ya kuzaliwa na alikuwa akienda nyumbani kwake ili kumshtukiza kwa zawadi ya mapema kabla ya siku yenyewe.

Kinuthia alimshukuru Mungu kwa kumlinda na kudokeza kwamab ilikuwa ajali ndogo tu na hakuna aliyejeruhiwa wala kuumia.

Katika video hiyo, Kinuthia alikuwa anacheza wimbo wa kutoka shukrani kwa Mungu kwa kumnusuru kutokana na ajali, kibao cha Joel Lwaga akimshirikisha Chris Shalom, Umejua kunifurahisha.

“Ni asubuhi mbaya sana hii ambapo nilikuwa nataka kumshtukizia mama yangu kwa zawadi ya mapema ya kumtakia heri njema ya siku yake ya kuzaliwa lakini nikapata ajali. Ahsante Mungu hakuna hata mmoja aliyejeruhiwa, lakini Mungu alidhibiti hali,” kinuthia aliandika kwenye video hiyo ikionesha magari mawili meusi, moja likidhaniwa kuwa lake yakiwa yamekwaruzana kidogo tu.

Kinuthia ni mwanablogu kwenye mtandao wa TikTok ambaye anaunda klipu akiwa amevalia kama mtoto wa kike na kujipodoa vizuri kwenye mwili wake wa kibonge unaowafanya wengi kuchanganyikiwa kufahamu kwa mara moja jinsia yake.

Mashabiki wake walimshukuru Mungu kwa kumsalimisha kutoka mkosi huo wa ajali na kumuombea kupata suluhu ya haraka kwa tatizo hilo kwani hawawezi kuwa na furaha pasi na kufurhia mitikasi yake kwenye TikTok.