(+video) Bintiye Mulamwah afurahisha kwa weledi kucheza densi ya wimbo wa Vaida

Carrol Sonie na bintiye Keilah walikuwa wakicheza video hiyo ambayo imewafurahisha wengi mitandaoni

Muhtasari

• “Lazima ningefanya hii pia nami lakini Keilah aliifanya vizuri zaidi kwa jinsi alivyoicheza ajabu,” Carrol Muthoni aliandika kwenye video hiyo Instagram.

Mashabiki katika mtandao wa Instagram wamefurahishwa na jinsi Keilah Oyando, mtoto wa mwigizaji Carrol Muthoni Sonie na mzazi mwenziwe, mchekeshaji Mulamwah alivyocheza densi kwa ngoma ya Kiluhya ya Vaida.

Mashabiki wengi walizua utani mkali kwamba mtoto huyo kwa jinsi alivyokuwa akicheza densi hiyo kabisa ni chembechembe za Kiluhya zilizopo ndani yake, wakimtania Mulamwah ambaye asili yake ni kutoka jamii hiyo.

Mwigizaji Carrol Sonie alisema kwamba naye alishawishika kufanya klipu hiyo akicheza densi wimbo wa Vaida amabo umetrend kwa takribani wiki mbili sasa mitandaoni.

Anaonekana akianza kucheza kabla ya bintiye Keila kujiunga naye na kuanza kuzikwenda kwa staili za kufurahisha macho.

“Lazima ningefanya hii pia na mi lakini Kweilah aliifanya vizuri zaidi kwa jinsi alivyoicheza ajabu,” Carrol Muthoni aliandika kwenye video hiyo Instagram.

Watu wali walifurahia na kusema kwamba mchekeshaji Mulamwah alikuwa anazungumza maneno ya hovyo kuhusu uzazi wa mwanawe ila kwa jinsi ile ni kweli kabisa asili yake haiko mbali na huko kwa kina Mulamwah.

“Uluhya uliopo ndani ya Keilah hakuja kufanya mzaha kwenye video hiyo,” mwingine aliandika huku akifuatisha na emoji za kucheka.

Hivi majuzi wakati mtoto Keilah alikuwa anafikisha umri wa mwaka mmoja tangu kuzaliwa, babake, Mulamwah aliibua ugomvi tena na Sonie kwa kumtuhumu kwamba anatumia mtoto huyo kama kitega uchumi mitandaoni.

Mulamwah tangu waachane na Sonie amekuwa akionekana kuwa na machungu na nongwa sana kwa kile wengi wanasema kwamba hapendi au hataki kabisa kumuona mama mtoto wake akiwa na furaha kwani ni kama jambo hilo humuuma sana na kuanza kutema utumbo mitandaoni.

Mulamwah katika ujumbe wa kumtakia heri njema ya kuzaliwa alidokeza pia kwamba huenda anatarajia mtoto mwingine kutoka kwa mama tofauti au tayari ana mtoto mwingine.