Grand P ateuliwa balozi wa utamaduni wa Guinea nchini Mali

Msanii huyo mbilikimo alifurahia kuteuliwa kwake na serikali ya Guinea huku akisema mataifa hayo mawili ni ndugu.

Muhtasari

• Asante  kwa Mheshimiwa Rais wa Mpito 🇬🇳 kwa kuzingatia 💪Mali na Guinea ni ndugu - Grand P.

Msanii wa Guinea Grand P
Msanii wa Guinea Grand P
Image: Facebook

Vyanzo vya habari kutoka nchini Guinea vinaarifu kwamba mwanamziki maarufu nchini humo mbilikimo Grand P ameteuliwa kuwa balozi wa utamaduni na utalii na serikali yake.

Msanii Grand P kupitia ukurasa wake wa Facebook alitangaza kwamba kanali Mamadi Doumbuya ambaye anashikilia wadhfa kama rais wa mpito kufuatia mapinduzi ya serikali miezi kadhaa iliyopita, alimteua kama balozi wa utamaduni katika taifa Jirani la Mali.

“Asante  kwa Mheshimiwa Rais wa Mpito 🇬🇳 kwa kuzingatia 💪Mali na Guinea ni mapafu mawili ya mwili mmoja. Heshima zote kwangu kuiwakilisha nchi yangu kama balozi wa utamaduni katika nchi ndugu #Mali🇲🇱 nikishirikiana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Guinea,” Grand P aliandika.

 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka bodi ya kitaifa ya watalii ya Guinea, Mheshimiwa Kanali Mamadi Doumbuya, Rais wa Mpito, aliripotiwa kumpatia pasipoti ya kidiplomasia kwa ajili ya kazi yake kama balozi wa utamaduni wa taifa hilo nchini Mali.

 

Grand P alimshukuru Mkurugenzi Mkuu na kusisitiza dhamira yake ya kufanya kazi kwa ajili ya kukuza Utamaduni na Guinea kama kivutio cha watalii.

Jina halisi la Grand P (Big P) ni Musa Sandian Kaba na alizaliwa mwaka wa 1990 huko Sanguiana, eneo la Kankan nchini Guinea.

 

Baadhi wamekuwa wakimzungumzia maumbile yake yasiyo ya kawaida ambapo anaonekana kama mtoto muda wote na gumzo hilo lilizidishwa hata zaidi baada ya kuweka wazi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanasosholaiti kutoka Ivory Coast, Eudoxie Yao ambaye ni mkubwa zaidi kwa muonekano wa mwili.