Jivunie mahali ulikotoka, Millicent Omanga atoa ushauri

Mheshimiwa huyo alionekana kuwa mwenye majivuno wa mabadiliko yake.

Muhtasari

•Picha hiyo ilionesha alivyobadilika Millicent, akiwa mwenye umri mdogo, kabla ya kuingia kwenye siasa na sasa.

Mabadiliko ya Millicent Omanga kabla na baada ya Siasa
Image: Caroline Mbusa

Mheshimiwa Millicent Omanga almaarufu Mama Miradi ameacha vinywa vingi wazi baada ya kuiweka picha yake ya zamani akiwa na mwanawe kwenye mtandao.

Picha hiyo ilionyesha maumbile yake yalivyobadilika, akiwa katika umri mdogo, kabla ya kuingia kwenye  ulingo wa siasa.

Mheshimiwa huyo alionekana kujivunia mabadiliko yake.

“Zoea kujivunia mahali umetoka,”alisema.

Chapisho hilo lilivutia wengi na kuwapa ari ya kufanya bidii kujiendeleza kwa siku za usoni.

Kabla ya kuingia siasa Omanga alisema alikuwa anauza shuka za mitumba alipokuwa akisomea Shahada yake katika chuo kikuu cha Nairobi.

Alisema kazi hiyo ilikuwa hatua kubwa maishani mwake. Alipata umaarufu wake wakati wa akiwa seneta maalum.

Mwanasiasa huyo aliwania kiti cha mwakilishi wa kike katika Kaunti ya Nairobi katika uchaguzi mkuu wa Agosti tarehe 9 kwa chama cha UDA  na kubwagwa chini na Esther Passaris wa ODM.

Alikubali kushindwa na hata kumpongeza Passaris aliyeshindaAliwashukuru wote waliompigia kura na wale ambao hawakumpigia kura.