Lil Baby adhibitisha kutumbuiza mashindano ya Kombe la Dunia Qatar

Mashindanohayovyatafanyika nchini Qatar kuanzia mwezi Novemba hadi Desemba mwaka huu

Muhtasari

• Gwiji huyo mwenye kipaji komavu ameimba albamu ya  ‘The World is Yours To Take'

Msanii huyo amedhibitisha kutumbuiza katka mashindano ya Kombe al Dunia
Lil Baby Msanii huyo amedhibitisha kutumbuiza katka mashindano ya Kombe al Dunia
Image: FACEBOOK//Lil Baby

Mwanamuziki maarufu kutoka Marekani Lil Baby  amedhibitisha kuwa atakua miongoni mwa wasanii wa kutumbuiza katika kipute cha kombe la duni cha mwaka huu nchini Qatar.

Lil Baby alijulikana sana mwaka wa 2017, kwa kibao chake kiitwacho ‘My turn’ na ‘Harder Than Ever.’

Mwanamuziki huyo akizungumza kwenye mtandao wake wa Tweeter, alidhihirisha kujawa na furaha,unyenyekevu na shukrani sufufu kwa nafasi hiyo ya kipekee.

Lil Baby alidhibitisha kuwa atarekodi wimbo mahususi kwa ajili ya mashindano ya kombe la Dunia ambayo yatang'oa nanga Novemba 20 hadi Desemba 18 huko Qatar.

Gwiji huyo mwenye kipaji komavu ndiye nguvu kazi nyuma ya albamu maarufu ya ‘The World is Yours To Take’ , albamu ambayo itachezwa kwenye mashindano hayo. Albamu hiyo ilitoka Septemba 23.

"Kombe la Dunia la FIFA hapa tunaenda," Lil Baby alisema.

Kwa wimbo huo, rapa huyo ameungana na wanachama wa Tears for Fears - Roland Orzabal na Curt Smith.

Kombe la dunia la mwaka huu litakuwa la kipekee kwani ndiomashindano ya kwanza tangu kuasisiwa kwa kipute hicho ambacho yatafanyika pasi na uwepo wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza aliyezikwa mapema wiki hii.

Ufaransa witajityoma ugani kwa lengo la kutetea ubiongwa huo ambao waliupata mnamo 2018 katika mashindano hayo yaliyofanyika Urusi.