Najihisi mwenye bahati kuwa na wewe mrembo - Kibenten wa Zari, Shakib Cham

Zari alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa Ijumaa.

Muhtasari

• “Furaha ya siku ya kuzaliwa Malkia wangu, siku hii iwe ya kweli na ya kushangaza kwako mrembo wangu! - Cham

Shakib Cham amsherehekea Zari
Shakib Cham amsherehekea Zari
Image: instagram

Mwanamitindo na mfanyibiashara Zari Hassan Ijumaa alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na watu mbalimbali walijumuuika naye kumtumia jumbe za heri njema.

Mmoja wa watu waliomtakia heri njema ni mpenzi wake mdogo Shakib Cham.

Kijana huyo ambaye hivi majuzi Zari alidokeza huenda ndiye mwanaume wake wa mwisho kuchumbiana na yuko tayari kumtolea mahari alimsifia Zari kwa ujumbe maridhawa akimtaja kama malkia katika himaya ya moyo wake.

“Furaha ya siku ya kuzaliwa Malkia wangu, siku hii iwe ya kweli na ya kushangaza kwako mrembo wangu! Nakupenda siku zote na daima na milele!! Najihisi kuwa na bahati kuwa na wewe mtoto,” Shakib Cham aliandika kwenye msururu wa picha za pamoja Instagram yake.

Zari hakutulia kwani alifika kwenye picha hizo na kumjibu kimahaba huku akisema kamwe hawezi kumuacha na kuwa anajihisi furaha na amani ya nafsi kuwa na yeye.

“Asante mpenzi wangu. Nakupenda sana babe❤️” Zari alimjibu.

Hivi majuzi Zari alijipata katika majibizano makali na watu mitandaoni waliokuwa wakimsuta kwa kuanza mahusiano na kijana mdogo ambaye amemuachqa kiumri mara dufu.

Zari alijitetea kwa dhana kwamba hata wanaume huwa na hulka ya kuingia kwenye mapenzi na wasichana wadogo kuwaliko kiumri na halijawahi kuwa tatizo lakini ikija kwa upande wa wanawake kuwa kimapenzi na vijana wadogo basi ni gumzo pevu.

Zari alitangaza kuwa kijana wake Cham ako tayari leo kesho kuongozana kuona wazazi wake na ikiwezekana kumtolea mahari kama mkewe pika pakua.