(+video) Mwanablogu Peace Loise (30) athibitisha kuwa bikira

Ningependa kuwazungumzia wanaume wote kule nje kujua kwamba sisi pia tuko - Loise.

Muhtasari

• Sisi ndio tulikuwa mpango mzima kitambo lakini sasa hivi huwezi pata mwanaume singo anayetaka kuchumbiana na sisi - Loise.

Mwanablogu wa mitandaoni nchini Kenya Peace Loise amejitokeza kimasomaso na kuzungumzia suala ambalo alisema wengi wa mashabiki wake wamekuwa wakilizungumzia kweney upande wa kutoa maoni.

Loise amesema kwamba ameamua kufunguka ukweli wake kwa vile ameona wengi wakiuliza swali hilo mara kwa mara anapopakia kitu kwenye mitandao yake ya kijamii.

Kulingana na Peace Loise, wengi wamekuwa wakimuuliza iwapo yeye ni bikra ama bado.

Katika video hiyo, Loise ameelezea ukweli wake kwamba yeye bado hajawahi kushiriki kitendo na mtu yeyote na kusisitiza bado yu bikra.

Alisikitika kwamab watu wengi siku hizi hawaamini kuwa kuna wanadada waliovunja uko lakini bado ni mabikra. Loise alisema hicho ndicho kilikuwa kigezo na kiwango cha mwanamke aliyejiheshimu zamani lakini sasa hivi hakuna hata mwanaume mmoja ambaye anaweza jitokeza kuwa tayari kuoa mwanamke bikra.

“Leo nimeamua kujikusanya na ujasiri wangu kuwazungumzia kuhusu suala ambalo wengi wengi mmekuwa mkinishinikiza niseme. Ndio ni kweli mimi ni bikra na sababu ambayo imenifanya kujitokeza ni kuwa nimegundua sisi (bikra) ni watu tuliotengwa katika jamii. Sisi ndio tulikuwa mpango mzima kitambo lakini sasa hivi huwezi pata mwanaume singo anayetaka kuchumbiana na sisi,” Loise alizungumza.

Alisikitika ni kwa nini heshima kwa bikra ilipotea na kusema watu kama hao wanafaa kutambuliwa na kuheshimiwa katika jamii.

“Tunafaa kuheshimiwa kwa sababu tumejilinda kuwa safi muda wote kwa ajili ya waume zetu wa siku za usoni. Ni jambo la kuumiza sana kupata kuwa jitihada zetu kujiweka safi hazitambuliki na mimi ningependa kuwazungumzia wanaume wote kule nje kujua kwamba sisi pia tuko,” Peace Loise alisema.

Peace Loise, 30, ni mpenda nywele asilia, mwanamitindo, muuzaji dijitali na MwanaYouTube. Mtayarishaji wa maudhui anayeishi Nairobi na ni miongoni mwa watu watano walioshinda shindano la Denri Face of Africa mnamo Januari 2021.