Wewe ni mtu mwingine bure kabisa - Butita amjibu mtangazaji

Alijibu hivyo alipoulizwa kuhusu kuachana kwake na aliyekuwa mpenzi wake Mammito Eunice.

Muhtasari

• Mimi niko sawa, maisha yangu yako sawa, niko sambamba na pia yeye ako sambamba - Butita alizungumzia kuachana na mpenzi wake Mammito.

Eddie Butita amjibu utumbo mtangazaji Ankali Ray
Eddie Butita amjibu utumbo mtangazaji Ankali Ray
Image: Instagram

Mzalishaji wa vipindi vya ucheshi ambaye pia ni mcheshi wa muda mrefu Eddie Butita amezua mjadala mitandaoni baada ya kusikika kwenye kituo cha redio moja ya humu nchini akijibu hovyo madai ya kutengana na aliyekuwa mpenzi wake, Mwigizaji Mammito Eunice.

Butita na Eunice walikuwa wapenzi wa muda mrefu kabla ya kuachana kimya kimya pasi na watu wengi kujua mitandaoni.

Wachache tu ndio walikisia kuwa huenda hali si shwari baina ya wapenzi hao wawili baada ya kila mmoja kumunfollow mwenzake mitandaoni, na hakuna aliyejitokeza wazi kusema kama ndio mwanzo wamevunja mahusiano yao.

Baada ya muda mrefu wa kukisia, Mammito Eunice mapema wiki hii akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja alisema kwamba yeye hayupo singo na wala hajawahi kuwa singo kwani pindi tu baada ya kuachana alifungua ukurasa mpya kimapenzi.

Kufunguka huku ndiko kuliwafanya wengi kutaka kusikia upande wa Butita katika hili na mtangazaji Ankali Ray alimtafuta kwa njia ya simu kutaka kujua kama ni ukweli ama ni utani wao tu maana wote ni wachekeshaji kiuhalisia.

“Lakini Ankali, vitu vingi vinafanyika Kenya, wewe uko tu hapo. Mimi niko sawa, maisha yangu yako sawa, niko sambamba na pia yeye ako sambamba. Namtakia mema kwa maisha yake. Mimi sina adui. Ankali wewe ni mtu mwingine, bure kabisa. Wewe ni mtu asiyefaa sana,” Butita alijibu kwa kero kubwa.

Alipolemewa na maswali, Butita alizidisha ukali wake dhidi ya mtangazaji na kumtaka kuamua ni swali ani kwanza anataka kuulizwa kabla ya kukata simu.

“Kaa chini uamue ni swali gani unauliza mtu. Una maswali mengi! Unataka ujibiwe nini? kwenda uko!” Butita alisema.