"Huwezi simamisha Reggae" Vera Sidika asutwa kwa kusema hawezi penda mtu wa Reggae

Sidika kwenye Insastory yake alisema kwamba hata yeye hawezi chumbiana na mtu anasikiliza miziki ya Reggae

Muhtasari

β€’ Ni kama mimi siwezi chumbiana na mtu anasikiliza Reggae - Vera Sidika.

Vera sidika asema hawezi chumbiana na watu wa reggae
Vera sidika asema hawezi chumbiana na watu wa reggae
Image: instagram

Mwanasosholaiti mstaafu Vera Sidika amedokeza kwamba yeye pia hawezi kujipata au hata kuwaza tu kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mtu ambaye anasikiliza miziki aina ya Reggae.

Mama huyo wa mtoto mmoja alikuwa akiyasema haya baada ya mtangazaji maarufu Kanene Goro kuweka wazi kwamba yeye ni vigumu kuchumbiana na mwanaume mwenye miziki yake ni ya Reggae.

Vera Sidika alipakia picha ya habari hizo na kusema kwamba mtangazaji huyo hayupo peke yake kwani wapo wanawake wengi nyuma yake ambao hawana mapenzi hata kidogo na watu wanaosikiliza miziki ya mitindo taratibu ya Reggae.

β€œHuyu ni kama mimi kabisaaa,” Vera Sidika alipakia kwenye instastories zake alizungumzia matamshi ya mtangazaji huyo.

Vera Sidika ni mamake mtoto Tajiri Asia Brown na ameolewa na mwanamuziki wa ngoma za kizazi kipya Brown Mauzo.

Baada ya Vera Sidika kutolea maoni hayo kumuunga mkono mtangazaji huyo, watu mbali mbali walishindwa kujizuia na walikuwa na maoni kinzani.

Wengine walimsuta kwa kuzungumzia mambo ya kuchumbiana na tayari yuko kwenye ndoa na msanii Mauzo pamoja na kuwa na mtoto juu huku wengine wakimtania kwamba watu wa rasta hata wao hawapendi kabisa kuchumbiana na wanadada mikorogo wa kujichubua.

β€œVera Sidika ako kwa ndoa na anaongea stori za kudateπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚dunia ni ngumu,” shabiki kwa jina Muriithi Caleb aliandika.