Wanawake wote duniani tuwaamini waume zetu - Mpenzi wa Stevo Simple Boy ashauri

Kuwa na mtuu ambaye anakuaminia maishani wewe kutunga nyimbo ili kunipa furaha maishani ni kitu kikubwa Sana - Mrs Stevo Simpe Boy.

Muhtasari

• Kwa kweli upo na uwezo mkubwa kufanya chochote duniani kwa Imani ya mungu na kuwa na mtuu ambaye anakuaminia maishani - Gee.

Stevo simple boy na mchumba wake Gee.
Stevo simple boy na mchumba wake Gee.
Image: instagram

Mrs Stevo Simple Boy kama anabyojiita ni mpenzi mpya wa msanii Stevo Simple Boy na miezi michache iliyopita walikuwa gumzo la vijiweni kwa kuvishana pete za uchumba.

Mwanadada huyo ambaye jina lake lingine ni Gee amemmiminia sifa tele msanii huyo kwa kumkubali kuwa mchumba wake na hata kuchukua pia nafasi hiyo kuwahimiza watu kwamba hata uwe wa hovyo aje yupo mmoja aliyeandaliwa mahususi kwa ajili yako.

Juzi baada ya kuachia wimbo mpya wa Wedding Day, msanii Stevo Simple Boy alizungumzia kilichomfanya kuandika wimbo huo wenye ujumbe wa kugusa.

Stevo alieleza kwa hisia kwamab wimbo huo aliutunga ili kuelezea ulimwengu kwamab hatimaye amepata wa kumpa mapenzi ya kweli baada ya muda mrefu wa kugeuzwa kinyago cha kuchekwa kutokana na maumbile yake.

Itakumbukwa Stevo mwaka 2019 alipochipuka na kibao chake cha kwanza kabisa cha Mihadarati wengi walimkejeli kutokana na maumbile yake na hata wengine kuanza kutumia sura yake kama meme. Alisema hata aliyekuwa mpenzi wake Pritty Vishy alimbwaga kwa sababu ya maumbile yake.

Sasa mpenzi wake mpya pia ameonekana kukubaliana naye na kuwahimiza watu kutowacheka wenzao kutokana na jinsi wanavyoonekana.

Kwa kweli upo na uwezo mkubwa kufanya chochote duniani kwa Imani ya mungu na kuwa na mtuu ambaye anakuaminia maishani wewe kutunga nyimbo ili kunipa furaha maishani ni kitu kikubwa Sana #weddingday,” mchumba wa Stevo aliandika kwenye Instagram.

Alizidi kuwausia kina dada kwamba uwezo upo wa kumpaka mwanaume ambaye hana chochote lakini ukiaminia katika safari ya maisha na umpende kwa kweli mwisho wa siku mtafanikiwa pamoja.

Unaweza Pata mwanaume Hana chochote lakini ukimwaminia na kumpa motisha atapata chochote mungu akuzidie na kwa wanawake wote duniani tuwaaminie wanaume zetu na tuwape motisha kikazi na kinyumbani ni watu wa maana wanapiga vita za kimaisha sababu yetu,” Mrs Stevo Simple alitoa ushauri.