Mwakilishi wa kike wa Bomet, Toto asherehekea kufikisha miaka 25

Toto alishinda uwakilishi wa kike Bomet akiwa na umri wa miaka 24 miezi michache iliyopita.

Muhtasari

• Toto alishinda uwakilishi wa kike Bomet kupitia tikiti ya chama cha UDA baada ya kupata kura Kura 242,775.

Toto asherehekea kufikisha miaka 25
Toto asherehekea kufikisha miaka 25
Image: instagram

Mwakilishi wa kike katika kaunti ya Bomet, Linet Chepkorir almaarufu Toto wikendi hii alisherehekea kufikisha umri wa miaka 25.

Toto ambaye alitajwa kuwa miongoni mwa wanasiasa wachanga na ambaye ndiye mdogo kabisa katika bunge la kitaifa ndio ilikuwa siku yake ya kuzaliwa kufikisha miaka 25 kwa mara ya kwanza katika maisha yake kama kiongozi kwenye bunge la kitaifa.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Toto alipakia picha yake ambayo imekuwa ikisumbua mitandaoni na kuwanyima wanaume usingizi, na kupasua mbarika kuwa ni siku yake ya kipekee kwani ndio amefikisha umri war obo karne.

“HERI YA KUZALIWA KWANGU. Asante Mungu kwa kutoniacha daima uendelee kunilinda,” Toto aliandika.

Malefu ya Wakenya walifurika kumtakia heri njema ya kuzaliwa huku wengine wakifagilia urembo wake unaopendeza wote wanaompenda na wasiompenda.

“Madam, siku ya kuzaliwa yenye furaha. Mwenyezi Mungu akubariki kwa amani, furaha na unyenyekevu ili uweze kuwatumikia watu wake vyema” mwanaume kwa jina Daniel Osogo Nyakina alimwandikia.

“Siku ya kuzaliwa yenye furaha na sabato yenye furaha, msichana mdogo. Wewe ni mfano wa kuigwa kwa wasichana wetu. Mungu aendelee kukulinda siku zote,” Lenis Zawadi ni mwingine ambaye aliandika ujumbe mtamu wa kumtakia heri njema.

Tangu kuteuliwa, Toto amekuwa ni gumzo mitandaoni haswa kutokana na umahiri na jitihada alizoweka mpaka kushinda tena kwa kutumia chama kikubwa ambacho alishinda mchujo pia.

Ijumaa Toto alikuwa miongoni mwa wanasiasa walioandamana na naibu rais Rigathi Gachagua kuelekea Kisumu kushuhudia hafla ya miziki ya shule nchini Kenya.

Toto alishinda uwakilishi wa kike Bomet kupitia tikiti ya chama cha UDA baada ya kupata kura Kura 242,775 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Dkt Alice Milgo wa Chama Cha Mashinani (CCM), aliyepata kura 43,180, akifuatiwa na Bi Beatrice Chepkemoi Chebomui aliyepata kura 4,639.

Wagombea wengine walikuwa Florence Cherono Birir (mgombea Huru) aliyepata kura 2,045, Viola Cherono Tesot (Independent akiwa na kura 1,740), Hellen Taplelei Rotich (Wiper kura 1,665), Jesca Cherono Rono (ANC kura 1,478) na Susan Korir (ODM kura 1,000). kura) kura 27), Susan Koech (Huru, kura 1,247).