"Mambo tu ya Mungu" - Maribe azungumzia fununu za kupata kazi kwa DP Gachagua

Kama alivyoiweka rafiki yake Maribe, Nzau ya Musau huko Twitter, Maribe ameweza kupata kazi katika ofisi ya Gachagua.

Muhtasari

•Jacque Maribe aliweza kushiriki kutoa maoni yake kuhusu madai hayo ila bado hajaweka wazi kama madai hayo ni ya kweli.

Jacque Maribe
Jacque Maribe

Aliyekuwa mwanahabari Jacque Maribe azungumzia fununu kuwa yeye ndiye Mkurugenzi anayekuja wa Mawasiliano katika ofisi ya Naibu wa Rais Rigathi Gachagua.

Kama alivyoiweka rafiki yake Maribe, Nzau ya Musau huko Twitter, Maribe ameweza kupata kazi katika ofisi ya Gachagua.

“Mkurugenzi wa Mawasiliano mtarajiwa katika ofisi ya Naibu Rais Rigathi Gachagua Jacque Maribe amejikusanya kiujasiri,” alisema Nzau.

Katika chapisho hilo, Nzau aliendelea na kusema Maribe ambaye awali alitupilia mbali ahadi ya kufunga pingu za maisha na Katibu mtarajiwa wa baraza la mawaziri la Kenya Kwanza, Dennis Itumbi, sasa huenda tena mwanablou huyo amekuja na ombi jipya kwake.

Jacque Maribe aliweza kushiriki kutoa maoni yake kuhusu madai hayo ili bado hajaiweka wazi kama madai hayo ni ya kweli.

Ni mambo ya Mungu tu,” Maribe alisema.

Alichapisha machapisho yaliyoandikwa na watu wengine kule Twitter akitoa maoni yake kuhusu suala hilo.

Baada ya madai haya Maribe aliweza kujikuta kweye kinyanganyiro cha babake mwanawe baada ya shabiki wake kutoa maoni.

Anafaa kufugua mashtaka ya baba ya mtoto wake ili aweze kupata pesa za kujikimu,” shabiki alisema.

Maribe aliweza kujibu maoni hayo na kusema hawezi jihusisha na masuala hayo ya uzazi.

Kwa nini nifunge mashtaka na nina hela zangu? Hizo ni vitu siwezi fanya,” alisema.

Hii ni baada ya kuwa Maribe alikuwa kweye hali ya huzuni na kuwa alikuwa ametumbukia kwenye ulevi chakari.

Maribe aliyakana madai hayo na kusema huwa hatilii maanani kilichomo mitandaoni kutafuta kiki kutumia jina lake ili kupata maoni kwa wanamitandao.

Aliongeza na kusema ako sawa, buheri wa afya na kuwa huwa habugii mvinyo.

Huzuni? Na nani? Lini? Kwa nini? Hua sinywi mimi. Nina afya njema na furaha,”alisema.