Akina mama tulioko singo, tunachoma kuenda na watoto wetu klabuni - Mwalimu Rachael

Upende usipende, heshima itadidimia kabisa na kupungua - Mwalimu Rachael

Muhtasari

• Lazima tujaribu kadri ya uwezo wetu sisi kama kina mama wachanga sasa - Mwalimu Rachael.

Mwalimu Rachael awasuta kina mama wanaoenda na watoto wao klabuni
Mwalimu Rachael awasuta kina mama wanaoenda na watoto wao klabuni
Image: Facebook

Mtangazaji wa redio Mwalimu Rachael amewazomea kina mama wanaoishi na watoto wao bila waume zao almaarufu Single Mothers. Rachael amewaambia kuwa wanachoma picha kutembea na watoto wao hadi sehemu za kuuza mvinyo na burudani.

Mtangazaji huyo alisema kwamba kina mama hao wengi wana tabia ya kutoka na watoto wao ambao wamefikisha umri wa miaka 18 kuenda juu na kuelekea nao sehemu za kujiburudisha kwa tafrija, suala amablo kulingana na yeye linaharibu heshima kati ya mtoto na mama mzazi kabisa pindi wanapolewa.

“Akina mama tulioko singo, tunachoma. Tumeona hili likitokea kwa kina mama wengi ambao ni singo, mama unatoka na mtoto wako ndio hatukatai amefikisha umri wa miaka 18 labda 22 hivi, mnaandamana kwenda klabuni,” Mwalimu Rachael alisema.

Alisema kwamba mama hao wanaharibu watoto wao kwani akina baba ambao ni singo ni nadra sana kuwapata wakifanya hivyo bali swala hili linatokea sana na kina mama singo.

“Kina baba wale singo hawafanyi hivi, hata wale amabo wameoa au wako katika hali nyingine hawafanyi hivi. Upende usipende, heshima itadidimia kabisa na kupungua. Lazima tujaribu kadri ya uwezo wetu sisi kama kina mama wachanga sasa, lazima mipaka ya heshima baina yetu na watoto idumu,” alisema.

Mtangazaji huyo alisisitiza kwamba wacha mtoto na mzazi wabaki kuwa marafiki wakati wote wako katika hali sawa bila kuhitilafiwa na ulevi. Huo ndio wakati pekee amabo mzazi anaweza mpa mtoto mawaidha yaliyo sawa pia.